CHAMA cha Mapinduzi (CCM)
kimewataka Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar kuendelea
kushirikiana ili kuunda nguvu ya pamoja itakayosaidia kuharakisha
maendeleo ya nchi kwa ufanisi zaidi.
Kimesema utendaji mzuri wa
viongozi hao ndani ya Baraza hilo ndiyo utakaoweza kukirahisishia kazi
Chama cha Mapinduzi katika uchaguzi mkuu wa 2020, hali itakayojenga
imani kwa wananchi kuirejesha tena CCM madarakati kutokana na utendaji
mzuri wa viongozi hao.
Akizungumza Naibu Katibu Mkuu wa
CCM Zanzibar, Nd. Vuai Ali Vuai wakati akibadilishana mawazo na Katibu
Mpya wa Kamati ya Wawakilishi wa Chama cha Mapinduzi ndani ya Baraza la
Wawakilishi Zanzibar (Mnadhimu) huko Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini
hapa.
Nd. Vuai alimpongeza kiongozi
huyo kwa kuaminiwa na Wajumbe wa Baraza hilo na kumchagua kuwa Mnadhimu
wa Wawakilishi wote wa CCM ndani ya Chombo hicho cha kutunga sheria za
nchi.
Alisema kuchaguliwa kwa Mnadhimu
huyo pamoja na msadizi wake kutasaidia kuongeza ufanisi wa kusimamia
vyema shughuli za baraza la wawakilishi ili ziende sambamba na mahitaji
ya wananchi majimboni.
Alieleza kwamba mbali na viongozi
hao kuwa na jukumu la kuandaa miswaada, kutunga sheria na kupitisha
Bajeti za nchi bado wana wajibu wa kusimamia kwa vitendo ilani ya
Uchaguzi ya CCM ya 2015/2020 pamoja na kulinda maslahi ya Chama hicho.
Tags
SIASA