| Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria mkutano huo wakifuatilia taarifa toka kwa Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage leo mjini Dodoma. |
(Picha zote na Benedict Liwenga, MAELEZO, Dodoma)
……………………………………………………………………………………………………..
Na Benedict Liwenga, MAELEZO, Dodoma.
JUMLA ya dola
Bilioni 3 za Kimarekani zinatarajiwa kutumika katika ujenzi wa Mgodi wa
Makaa ya Mawe na Chuma wa Liganga na Mchuchuma.
Kauli hiyo
imetolewa Leo mini Dodoma na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji,
Mhe. Charles Mwijage wakati akiongea na Waandishi wa habari mini Dodoma.
Amesema mradi
huo unaojengwa kwa ubia kati ya Tanzania Kupitia Shirika la Maendeleo la
Taifa (NDC) na Kampuni ya China ya Sichuan Hongda Group unatarajia
kuanza mwaka huu.
Mhe. Mwijage
amesema kuwa fedha za kuwalipa fidia wananchi wanaozunguka maeneo ya
mradi huo ziko tayari ambapo zinatarajiwa kutumika zaidi ya bilioni 13
kwa ajili ya fidia na makazi.
Alisema kuwa
kukamilika kwa mradi huo kutasadia kuzalisha umeme Megawati 600 ambapo
250 zitatumika katika Kiwanda cha Chuma na nyingine 350 zitapelekwa
kwenye Gridi ya Taifa kwa ajili ya kuongeza nguvu katika nishati ya
umeme.
‘’Pamoja na
kuchimba chuma, Mradi wa Mchuchuma na Liganga utahusisha ujenzi wa Kinu
cha Umeme chenye uwezo wa Megawati 600”, alisema Mhe. Mwijage.
Ameongeza
kuwa, Tanzania kwa sasa itakuwa na umeme wa gesi, maji na umeme wa makaa
ya mawe ambapo umeme wa makaa ya mawe utakuwa msaada mkubwa kwa nchi
kwani hautegemei tabianchi kama ilivyo vyanzo vingine vya umeme.
Mhe. Mwijage
amesema kuwa katika mradi huo, Tanzania itakuwa na hisa asilimia 20 na
Mwekezaji kutoka China atakuwa na asilimia 80, lakini hisa za Tanzania
zinaweza kuongezeka hadi kufikia 45.
Chini ya mradi
huo, Mwekezaji huyo anatakiwa kutoa elimu kwa Vijana katika ngazi zote
za teknolojia zitakazohusika kutengeneza mgodi huo.
‘’Tutafundisha
vijana wetu kwa ngazi tofauti kwani kampuni hii ni ya ubia kati ya
Tanzania na China, tuna mamlaka sawa, tuna Wakurugenzi wetu wa Tanzania
ndani ya hiyo kampuni, kwahiyo tutashiriki na hatutakuwa watazamaji”,
alisema Mhe. Mwijage.
Kwa upande
wake Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge inayosimamia Viwanda, Biashara na
Uwekezaji ambaye pia ni Mtaalam katika masuala ya madini, Mhe. Dkt.
Dalaly Kafumu amesema kuwa, lengo la kuwajengea makazi wakazi wa maeneo
ya mradi huo ni kuwawezesha wakazi hao kuwa na uhusiano mzuri na mgodi
unaotarajiwa kujengwa.
‘’Serikali
imeamua kuwajengea makazi wananchi ambao wanazunguka mradi Ili kuepusha
wakazi hao kutumia pesa watakayolipwa kama fidia kwa matumizi mengine na
kukosa makazi baadaye kuja kuilaumu Serikali kwamba imewadhulumu kwa
kutowapa pesa za kutosha za kujenga nyumba”, alisema Dkt. Kafumu.
Tags
HABARI KITAIFA