…………………………………………………………………………………………………
Na: Geofrey Tengeneza
Bodi mpya ya Wakurugenzi wa TTB
iliyoteuliwa hivi karibuni imekutana leo katika ofisi za TTB jijini Dar
es salaam katika mkutano wake wa kwanza toka iingie madarakani.
Mkutano huo ambao ulikuwa mahsusi
kwa ajili ya wajumbe wa Bodi hiyo kufahamu zaidi kazi na majukumu ya
Bodi ya Utalii Tanzania(TTB) ulifanyika chini ya uenyekiti wa Jaji
Mstaafu Thomas Mihayo na kuhudhuriwa pia na Menejimenti ya TTB.
Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii
Tanzania Bi Devota Mdachi alitumia pia mkutano huo kuwatambulisha
wajumbe wa Menejimenti ya TTB kwa Mwenyekiti na Wakurugenzi hao wa Bodi.
Bodi ya wakurugenzi iliyoteuliwa mwezi Mei mwaka huu ina wajumbe sita
ambao ni Bw. Ibrahimu Mussa ambaye ni Mkurugenzi wa Masoko na Utalii wa
TANAPA; Balozi Joseiph Sokoine , Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika
katika Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki, Ushirikiano wa
Kimataifa na Kikanda; Bw. Mark Leveri, Mtaalamu wa filamu na matangazo.
Wengine ni Bw. Richard
Rugimbana, Bw. Richard Rugimbana, Mtendaji Mkuu wa Shirikisho la Vyama
vya Utalii Tanzania (TCT), Bibi Zubein Muhaji Mhita, Bibi Zabein Muhaji
Mhita, Mbunge Mstaafu na Mkurugenzi wa Elimu ya Msingi Msataafu na Bw.
Agustine Kungu H. Olal, Kamishna Msaidizi wa Sera na Uchumi, Wizara ya
fedha na Mipango. Mjumbe mwingine ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa TTB
Devota Mdachi ambaye pia ni Katibu wa Bodi hiyo ya Wakurugenzi.
Mwenyekiti na Wajumbe hao wa Bodi
ya Wakurungenzi wa TTB watakuwa madarakani kwa miaka mitatu kuanzia
tarehe 24/04/2016 hadi tarehe 23/04/2019 .
Tags
HABARI KITAIFA