Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa
Kaunda suti) akiwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoani humo, Ahmed Msangi
(wa tatu kushoto) pamoja na askari wengine wa jeshi hilo, wakiyaangalia
mapango ya utemini, jijini Mwanza ambako kulifanyika operesheni ya
kupambana na majambazi baada ya majambazi hao kufanya mauaji katika
msikiti wa Rahmani uliopo Kata ya Mkolani jijini humo. Picha na Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wa pili
kushoto) akimuuliza jambo Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoani Mwanza, Ahmed
Msangi (kushoto) wakati walipokuwa wanawasili msikiti wa Rahmani mkoani
humo uliovamiwa na majambazi na kuua waumini watatu ndani ya msikini
huo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wa pili
kulia) akimsikiliza Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi
(kulia) wakati walipokuwa wanatoka msikitini mara baada ya kuzungumza na
waumini wa msikiti huo wa Rahmani mkoani humo. Msikiti huo ulivamiwa na
majambazi hivi karinbuni na watu watatu waliuawa. Picha na Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mzee
wa Msikiti wa Rahmani uliopo Mkolani, jijini Mwanza, Abeid Gati
(kushoto), akimpa fedha mke wa mmoja wa watu waliouawa na majambazi
ndani ya msikiti huo. Fedha hizo zilitolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa Kaunda suti) ikiwa ni
rambirambi yake kwa wafiwa wote watatu ambao walipoteza wenza wao katika
mauaji hayo. Hata hivyo Naibu Waziri alisema Serikali imesikitishwa na
tukio hilo la kikatili na pia jeshi lake lipo makini na linaendelea
kulinda usalama wa wananchi na mali zao. Picha na Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa
Kaunda suti) akitoka kukagua nyumba za makazi ya askari Polisi zilizopo
katika Kambi ya Mabatini jijini Mwanza, nyumba hizo zimetengewa fedha
kwa ajili ya kumMzee wa Msikiti wa Rahmani uliopo Mkolani, jijini
Mwanza, Abeid Gati (kushoto), akimpa fedha mke wa mmoja wa watu
waliouawa na majambazi ndani ya msikiti huo. Fedha hizo zilitolewa na
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa
Kaunda suti) ikiwa ni rambirambi yake kwa wafiwa wote watatu ambao
walipoteza wenza wao katika mauaji hayo. Hata hivyo Naibu Waziri alisema
Serikali imesikitishwa na tukio hilo la kikatili na pia jeshi lake lipo
makini na linaendelea kulinda usalama wa wananchi na mali zao. Picha na
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto)
akimpa pole askari Polisi, Mageni Kaseha aliyepigwa risasi ya mguu na
majambazi wakati wa mapambano kati ya polisi na majamabazi hao katika
mapango ya utemini, jijini Mwanza. Askari huyo amelazwa katika Zahanati
ya Jeshi hilo iliyopo katika Kambi ya Mabatini, jijini humo. Picha na
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto)
akizungumza na askari polisi katika Kambi ya Mabatini jijini Mwanza,
ambao walipambana na majambazi na kufanikiwa kuwakamata wakati wa
operesheni hiyo. Majambazi hayo yalijificha katika mapango ya Utemini
jijini humo na ndipo yakavamiwa na polisi mara baada ya kuvamia msikiti
wa Rahmani uliopo Mkolani jijini humo na kufanya mauaji. Masauni
aliwapongeza askari hao kwa kupambana na majambazi hayo na kuwasisitiza
kuwa kazi bado inaendelea wazidi kupambana mchana usiku ili wananchi
waweze kuishi kwa amani. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella kimpa taarifa ya hali ya usalama
mkoani humo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad
Masauni (wa tatu kulia) wakati kiongozi huyo wa Wizara alipofanya ziara
mkoani humo. Katika ziara yake, Masauni alitembelea mapango ya Utemini
mkoani humo ambapo mapambano kati ya polisi na majambazi yalifanyika,
pia alienda kuuona msikiti wa Rahman uliovamiwa na majambazi, pia
alizungumza na wafiwa na baadaye akamaliza ziara yake kwa kuzungumza na
askari polisi ambapo aliwapa pongezi kwa kazi nzuri ya kupambana na
majambazi hao. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.