Meneja
Msaidizi wa Chapa ya Coca – Cola, Mariam Sezinga, akizungumza na
waandishi wa habari kuwaelezea juu ya safari ya mchezaji Musa Said
anayetarajia kuondoka Jumatano ya Juni 28, 2016 kwenda nchini Ufaransa
kwenye kambi ya kimataifa ya Copa Coca-Cola. Pembeni ni Katibu Mkuu wa
Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohamed Kiganja, Mchezaji Musa Said
Bakari na Mwalimu wake wa Kibasila.
Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
—
Na Devotha Kiwelo.
—
Na Devotha Kiwelo.
MCHEZAJI
bora wa mashindano ya UMMISETA yaliyofanyika mwaka jana mkoani Mwanza,
Said Musa Jumatano ya Juni 28, 2016 kuelekea Ufaransa katika kambi ya
Kimataifa ya Copa Coca – Cola ambayo imeandaliwa na kampuni ya kinywaji
cha Coca – Cola .
Akizungumza
jijini Dar es Salaam katibu mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT),
Mohamed Kiganja alisema udhamini wa kampuni ya Coca – Cola imetambua
umuhimu wa michezo hivyo kukubali kudhamini michezo kupitia shule za
sekondari ili kukuza vipaji vya wanamichezo chipukizi ambao wanamalengo
makubwa katika kuitumikia nchini yao kupitia michezo.
“Kwetu
sisi imekuwa faraja kwa kuibua kipaji kichanga ambacho kitakuwa ni
mfano wa kuigwa kama ilivyo kwa Samatta ambaye amekuwa kioo kwa jamii ya
wanamichezo na hivyo kuomba makampuni mengine kujitokeza kwa ajili ya
kusaidiana na Coca – Cola”, alisema.
Kiganja
alimtaka Musa kuzingatia nidhamu kipindi chote atakachokuwepo kwenye
kambi ili kujijengea heshima katika kukuza kipaji chake kwa kipindi
chote ambacho atakuwa chini ya walimu wageni ambao hajawahi kukutana nao
na hiyo italeta heshima nchini.
Kwa
upande wa Meneja msaidizi wa chapa ya Coca – Cola, Mariam Sezinga,
alisema wamefurahi kupata nafasi ya kudhamini mashindano hayo kwa kuwa
ndiyo mara yao ya kwanza na imefanikiwa kufikia malengo ya kupata
mchezaji ambaye atakuwa muwakilishi wa Tanzania katika kambi ya
Kimataifa ya Copa Coca – Cola iliyopo jijini Paris nchini Ufaransa.
Alisema
Musa ataondoka kwa kupitia Nairobi kwa kuwa kozi inaanza kesho na
kumalizika Julai 4, hivyo aliwataka wanafunzi wengine kujituma ili
kufikia malengo kama aliyofikia Mussa.
“Sisi
kama kampuni imekuwa ni faraja kwani tutakuwa tumeitangaza nchini kwa
kupitia Mussa na hii itakuwa ni muendelezo katika michezo
inayoendelea,”alisema.
Mussa
ni mwanafunzi wa shule ya sekondari Kibasila ambaye alizaliwa Agosti
11, 2000 huku akiwa ni mchezaji tegemeo katika timu ya shule na Mkoa wa
Temeke ambapo walitumia jina hilo kwa kupitia michezo.
Tags
MICHEZO KITAIFA