Mufti wa Tanzania, Sheikh Mkuu, Abubakary Bin Zubeir (kushoto) akiwa na
viongozi mbalimbali wa Baraza Kuu la Waislam Tanzania (Bakwata), wakati
wakimsubiri kumpokea, Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi, kuwasili
kwenye Ofisi za Bakwata Kinondoni Jijini Dar es Salaam, leo katika hafla
ya kumpongeza Mwanazuoni kutoka Kondoa,Tanzania, Sheikh Rajay Ayub
ambaye ameibuka mshindi wa kwanza Afrika na wa sita Duniani katika
mashindano ya 37 ya Kimataifa ya usomaji Qur-an kwa njia ya Taj-weed,
yaliyofanyika mwezi uliopita nchini Iran. Zifuatazo ni picha kem kem za
hafla hiyo.
About Bashir Nkoromo
Tags
HABARI ZA DINI






































