Na Peter Mkwavila,Dodoma.
TUME
ya Taifa ya uchaguzi jana ilikabidhiwa eneo la kiwanja na Mamlaka ya
Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA) kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya
makao makuu ambayo itakuwa mjini hapa.
Akizungumza
jana mara baada ya kukagua eneo la ekari 10 ambalo litatumika kujenga
ofisi hizo Mwenyekiti wa Tume ya taifa ya uchaguzi Jaji Mstaafu Damian
Lubuva alisema sasa tume inaenda kufikia lengo lake la kuwa na ofisi
Mjini Dodoma.
Alisema
ofisi yake pamoja na makamishna wa tume wamefika hapokwa ajili ya
kuliona eneo hilo la kiwanja na tumeridhika na tutakinunua kwa Sh.
Milioni 470 kama tulivyoelezwa na CDA wenyewe.
Alisema
lengo hilo lilikuwa la muda mrefukuwa na jengo la kutosheleza mahitaji
kwani sasa ofisi ya tume hiyo iliyooo jijini Dar es Salaam ina ofisi
tatu maeneo matatu tofauti lakini sasa wanatakiwa kufanya kazi eneo
moja.
Alisema katika uchaguzi unaokuja watafanya shughuli za usimamizi wakiwa mjini Dodoma.
Naye
Afisa Uwekezaji CDA, kwa upande wake Abeid Msangi alisema tume hiyo
imepatiwa kiwanja cha ekari 10 ambacho kimezungukwa na barabara ya lami
pande zote.
Alisema
tume ya taifa ya uchagui wameleta maombi yao na mamlaka ya ustawishaji
wa makao makuu imewapatia kiwanja eneo la uwekezaji la Inumbu lililopo
Njedengwa na kwenye eneo hili lina miundombinu yote, maji umeme na
barabara na sasa tunawaandalia hati.
Alisema
jumla ya ekari 1500 zimetengwa katika eneo hilo na kuwekewa miundombinu
mingine na kuzitaka ofisi za serikali kwenda CDA kutafuta maeneo kwa
ajili ya kujenga ofisi zao.
Kwa
upande wake mkurugenzi wa uchaguzi wa tume hiyo, Kailima Ramadhani
alisema katika uchaguzi mkuu uliopita walibakiza fedha kiasi cha bilioni
12 ambazo walimrudishia rais John Magufuli kwa ajili ya matumizi
mewngine lakini lengo lilikuwa ni kujibana ili wawe na ofisi zao.
Alisema Rais Magufuli alitoa wazo la wao kuhamia Dodoma ili watekeleze maleng ya serikali kuhakia Dodoma.
Alisema
eneo hilo lina miundombinu yote na wameanza mazungumzo la Wakala wa
majengo (TBA) ili ifikapo Oktoba uenzi uanze na baada ya mwaka moja
tuyme iwe na jengo lake
Mtendaji
Mkuu wa TBA, Elius Mwakalinga alisema kama wakala na msimamizi mkuu wa
majengo ya serikali watashirikiana na tume kuona azma yao inatimia.
Mwisho
Tags
HABARI KITAIFA
