BANDA MEDIA BLOG

HATA ULAYA WANAMJUA JERRY NA MAGUFULI – MURO


IMG_0004
Kufungiwa mwaka mmoja kujishughulisha na masuala ya soka hakumnyimi Jerry Muro kuishangilia timu yake ya Yanga, na alifanya hivyo wakati wa mchezo wa kimataifa wa kombe la shirikisho Afrika dhidi ya Medeama ya Ghana.

Akiwa amekaa kwenye eneo maarufu linalotumiwa na na shabiki maarufu kwa jina la Ally Yanga, Muro alikuwa ameshika bendera kubwa akiipeperusha kui-support timu yake iliyoambulia sare ya kufungana goli 1-1 katika mchezo huo.
“Baada pambano hilo kumalizika Muro alizungumza maneno haya: “Mchezo ulikuwa mzuri na kila kitu kilikwenda vizuri tunashukuru, mambo ndiyo kama mlivyoona aliyepata kapata na aliyekosa kakosa maisha yanaendelea,”alisema Muro ambaye kabla ya kufungiwa alikuwa kwenye mvutano mkubwa na shirikisho la soka nchini TFF.
“Hatuna kingine, ningekuwa msemaji wa Yanga ungekuta nazungumza lakini mimi nazungumza kama mdau wa mpira.”
Muro akazungumzia maisha yake mapya ya kifungo cha mwaka mmoja kutojihusisha na masuala yanayohusu soka ambapo alisema kwa sasa umaarufu wake umezidi kukua ukilinganisha na mwanzo kwasababu kila kona anazungumziwa yeye.
“Sasahivi nimekuwa maarufu sana, maana nchi nzima ni Jerry hata Ulaya wanamjua Jerry na Magufuli, zamani nikizungumza nilikuwa nazungumza kama msemaji wa Yanga, lakini sasahivi watu wanauliza huyo Jerry ni nani mbona anatingisha vigogo na kuhoji CV za watu?.”

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG