Beki wa kulia wa Yanga Juma Abdul amesema tiku yake haukucheza kwa style yao iliyozoeleka kutokana na wachezaji kuwa kwenye tension kubwa ya kutafuta matokeo kwenye mchezo wao dhidi ya Medeama.
Abdul ambaye anawania tuzo ya mchezaji bora wa msimu uliopita ameongeza kuwa, wapinzani wao pia walijipanga kushinda mchezo huo kitu ambacho kilizidi kuifanya mechi hiyo kuwa ngumu kwa upande wao.
“Sidhani kama tulicheza vizuri kwasababu tulikuwa na tension kubwa ya kutafuta ushindi kwa aina yoyote na ndiyo maana hatukuweza kucheza mpira tuliozoea siku zote,” alisema Juma ambaye majeruhi yalimfanya kukosa mchezo wa kwanza hatua ya makundi wakati timu yake ilipofungwa 1-0 na MO Bejaia.
“Mchezo ulikuwa mzuri kwa ujumla kwasababu hata jamaa wenyewe walikuwa wamejipanga kuja kushindana na ndiyo maana kama mnavyoona wamepambana na kuweza kutoka na pointi moja.”
“Ni jukumu la mwalimu kuweza marekebisho, siku zote sisi tunatengeneza nafasi nyingi tunashindwa kuzitumia kwahiyo mwalimu ameshaona udhaifu uko wapi na atafanyia kazi.”
Tags
MICHEZO KIMATAIFA