Soka ni moja ya michezo maarufu zaidi ulimwenguni ambapo wachezaji huvuna mamilioni ya fedha. Kutokana na hali hiyo wachezaji humiliki mali nyingi yakiwemo magari ya kifahari ambayo hutokana na pesa nyingi wanazoingiza.
- Neymar : Audi R8 GT
Nyota huyu wa Barcelona ni moja ya wachezaji wanaoingiza pesa nyingi
kwa sasa na kumiliki magari ya kifahari! moja ya magari hayo ni Audi R8
GT!
- Zlatan Ibrahimović : Porsche 918 Spyder
Mchezaji huyu wa zamani wa PSG na Sweden anassemekana kuwa na
majivuno ya hali ya juu kutokana na majibu yake ambayo hutoa kwa
waandishi. Alikuwa ndio mchezaji mwenye gharama kubwa klabuni hapo na
kumiliki gari lenye thamani kubwa zaidi ya wenzake aina ya Porsche 918
Spyder.
- Samuel Eto’o : Bugatti Veyron
Mchezaji huyu wa kimataifa wa Cameroon ni moja ya wachezaji matajiri
zaidi Afrika na ndio maana si ajabu kumwona akiendesha gari la thamani
kuliko hata wachezaji wengi maarufu ulimwenguni aina ya Bugatti Veyron.
- Karim Benzema: Bugatti Veyron
Mfaransa huyu ni moja ya wachezaji wanaoishi maisha ya kifahari
ulimwenguni. Amekuwa mchezaji tegemeo wa Real Madrid kwa muda mrefu
sasa. Anamiliki Bugatti Veyron, ambalo alinunua mwaka jana.
- Cristiano Ronaldo : Bugatti Veyron
Cristiano Ronaldo kwa sasa tunaweza kusema ndiyo mchezaji anayeongoza
kwa kuoenda maisha ya kifahari. Anamiliki magari 19, yakiwemo
Lamborghini Aventador LP 700-4, BMW M6, Bentley Continental GTC, na
Ferrari 599 GTB Fiorano. Hii ni picha ya aliyepigwa wakati akiendesha
Bugatti Veyron yake.
- Buggatti Veyron : Bugatti Veyron 16.4 Grand Sport Vitesse
Portugal wamebeba ndoo ya Euro 2016 hivi juzu-juzi, na naodha wao
Cristiano Ronaldo akaamua kujizawadia gari mpya aina ya Bugatti Veyron
16.4 Grand Sport Vitesse ili kujipongeza na ubingwa huo. Gari hilo
linagharimu dola mil 1.7 na lina uwezo wa kwenda maili 255 kwa saa.
Tags
MICHEZO KIMATAIFA