
Jose Mourinho kwa mara ya kwanza jana alisimama kama kocha wa
Manchester United kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Wigan Wigan
Athletic na kushuhudia timu yake ikipata ushindi wa mabao 2-0, magoli
yaliyofungwa na Will Keane na Andreas Pereira.
Haya ndio mambo manne makubwa yalioonekana kutokana na mchezo wa jana.
- Aina yake ya Staili ya uchezaji imeanza kuonekana
Licha ya kwamba huo ndio ulikuwa mchezo wa kwanza kama kocha wa
Manchester United, lakini tayari kumeokana viashiria vya aina yake ya
mchezo katika timu hiyo. Walikuwa wanamiliki mpira kidogo huku wakitumia
mfumo wa 4-2-3-1 ambao pia ulikuwa ukitumiwa na kocha wa zamani wa
klabu hiyo Louis van Gaal lakini utofauti ulikuwepo kwenye tempo ya
mchezo. Jana mchezo ulikuwa kwenye tempo ya hali ya juu. Wachezaji
walikuwa na uhuru mwingi lakini vile vile aina ya mashambulizi yalikuwa
ni ya moja kwa moja, na pia baadhi ya wachezaji walionekana kuwa nguvu
kubwa kama Ander Herrera.
Baada ya mchezo Mourinho mwenyewe alionekana kuanza kuwakubali
wachezaji wake na kusema kwamba wachezaji wanaonesha kuelewa
anachowaelekeza.
- Henrikh Mkhitaryan anaweza kuchezeshwa namba 10 ya kudumu
Watu wengi walikuwa wakitupia macho kwa wachezaji wapya hasa Henrikh
Mkhitaryan. Licha ya kukosa goli la wazi lakini alionekana kuonesha
uwezo wa hali ya juu. Mipira yake mingi ilionekana kuwa na hatari,
alikuwa akizunguka sehemu zote za uwanja…kulia, kushoto na katikati.
Ikumbukwe huyu ndiyo mchezaji aliyeongoza kwa kupiga pasi nyingi za
mabao msimu uliopita kwenye ligi ya Bundesliga wakati akicheza Borussia
Dortmund.
- Luke Shaw anaonekana kumvutia bosi wake mpya.
Baada ya kukaa nje kwa miezi 10 kutokana na jeraha mguu, Luke Shaw
alionekana kutokuwa na woga na kupandisha timu wakati akicheza beki ya
kulia.
Zaidi ya hapo Mourinho alimsifu sana baada ya kuamua kuahirisha
kwenda mapumzikoni na kuamua kufanya mazoezi kwa bidii ili kurejea
katika ubora wake wa awali baada ya kukaa nje kwa muda mrefu.
- Juan Mata alikuwa na mchango mkubwa licha kuingia kipindi cha pili
Katika kikosi cha kwanza kilichotajwa katika mchezo dhidi ya Wigan
hapo jana, jina la Mata halikuwepo na kwamba Mourinho alimuanzisha
benchi. Katika mabadiliko aliyofanya kipindi cha pili, Mourinho
alimuingiza Mata na kutoa pasi ya goli la kwanza lililofungwa na Will
Keane baada ya kuunasa kwa umaridadi wa hali ya juu mpira uliokuwa
ukipigwa na kipa wa Wigan kwenda kwa beki wake.