Lucia Swartz akiongea na wafanyakazi
Wafanyakazi wakifuatilia majadiliano wakati akizungumza nao.
Mfanyakazi wa TBL Group akiuliza swali
Baadhi ya wafanyakazi wakiwa katika picha ya pamoja na Lucia Swartz
…………………………………………………………………………………..
Akutana na wafanyakazi wa TBL Group
Mkurugenzi wa kitengo cha
Raslimali watu wa kampuni ya SABMiller kanda ya Afrika,Lucia Swartz,
yuko nchini kwa ziara ya kikazi ambapo amekutana na wafanyakazi wa
kampuni ya TBL Group ambayo ni kampuni tanzu ya kampuni hiyo.
Lucia Swartz amekutana na
wafanyakazi katika hoteli ya Holiday Inn iliyopo jijini Dar es Salaam
ambapo pia alipata fursa ya kufahamiana nao na kubadilishana mawazo
kuhusiana na masuala mbalimbali ya kuboresha ustawi wa wafanyakazi
ambapo pia walipata fursa ya kuuliza masuala mbalimbali yanayohusiana na
utawala na utendaji wa kazi za kila siku.
Tags
BIASHARA