Kundi la muziki wa Bongo linaloundwa na wadada wakali watatu likijulikana kama ‘The Scorpions ‘ limealikwa kutpiga show kesho kwenye Uganda Entertainments Awards.
Wadada wanaounda kundi la The Scorpions ni pamoja na Baby Madaha, Kabula na Bela Fasta. Manager anayesimamia kundi hilo ni Mama Lolla.
Kundi la The Scorpion limedhamiria kufanya kweli kitaifa na kimataifa kuhakikisha muziki wa Bongo unavuka mipaka ya Tanzania na kwenda mbali zaidi huku wao wakilenga kupata mafanikio makubwa kama kundi.
Pemba Sports Africa imeamua kuwa-promote wadada hao ili nao watoke na waendelee kimataifa. Kuna mipango na mikakati mikubwa kuhakikisha The Scorpions inasonga mbele na kuikia ndoto zake ikiwa chini ya Pembe Sports Africa.
Tags
KIBURUDANI