BANDA MEDIA BLOG

YANGA KUIFATA MAZEMBE JUMAPILI KUKAMILISHA RATIBA

IMG_0275Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Yanga SC wanatarajiwa kufanya mazoezi kesho Ijumaa na Jumamosi kwaajili ya kujindaa na mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi Kombe la Shirikisho dhidi ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Baada ya programu hiyo ya mazoezi ya siku mbili, timu hiyo itaondoka Jumapili usiku tayari kwa mchezo huo wa kundi A, ambao kwao ni wa kukamilisha ratiba utakaopigwa jijini Lubumbashi Jumanne saa 8:30 za mchana.

Yanga hata ikishinda mchezo huo haitakwenda kokote kutokana na kuwa na alama ambazo haziwezi kumfikia mshindi wa pili kwa sasa ambaye ni Medeama.
Leo kutwa nzima wachezaji wa Yanga wamekuwa na mapumziko kufuatia mchezo wa jana wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam, ambapo walipoteza kwa changamoto ya mikwaju ya penati 4-1 baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 ndani ya dakika tisini.
Waamuzi watakaocheza mchezo huo ni Helder Martins De Carvalho wa Angola ambaye atasimama katikati, akisaidiwa na waamuzi wasaidizi Jean Claude Birumushashu wa Burundi na Arsenio Chadreque Marengula wa Msumbiji.
Maofisa watakaohusika kwenye mchezo huo ni Antonio Muachihuissa Caxala (Angola), Gerges Rodolphe Bibi (Ushelisheli), Ali Mohamed Ahmed (Somalia) na Russell Paul (Afrika Kusini)
Yanga wanashika mkia kwenye kundi lao wakiwa na alama 4, huku TP Mazembe wakiwa kileleni na alama zao 10 ambapo wao ni kama tayari wamefuzu tu.
Medeama ya Ghana inashikilia nafasi ya pili na alama zao nane na Waarabu wa Algeria MO Bejaia wanashika nafasi ya tatu na pointi zao tano.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG