BANDA MEDIA BLOG

HATIMAYE MSAADA WA VIDEO WATUMIKA KWENYE MECHI YA SOKA


VIDE
Katika kuendelea kwa teknolojia, michezo mara nyingi imekuwa sehemu ya mafanikio ya maendeleo ya teknolojia hiyo katika kurahihisha maamuzi ndani ya viwanja vya michezo.

Tofauti na michezo mingine, upande wa soka umekuwa mgumu na imeshuhudiwa mabadliko yakija taratibu sana ukilinganisha na michezo mingine ambayo imekuwa ikiwekeza katika teknolojia zaidi kuliko kutegemea watu ili kuondoa matukio yenye utata.
Baada ya goli la Lampard pale Afrika ya Kusini kwenye kombe la dunia kukataliwa, iliinua hisia juu ya kuhitajika kwa teknolojia ya mstari wa goli “goal line technology” ambayo ilikuja kukubalika na kuanza kutumika katika ligi nyingi kubwa isipokuwa tu kwa mashindano yanayosimamiwa na shirikisho la soka barani Ulaya yaani UEFA.
Katika michezo mingine kama mpira wa kikapu, Baseball na mpira wa Marekani (American Football) na michezo kama Hockey, matumizi ya kamera maalumu zinazorekodi matukio uwanjani imekuwa msaada maalumu katika kutoa maamuzi na kupunguza mzigo kwa waamuzi.
Hili lilikuwa ni jambo linalosubiriwa katika soka na sasa limefika. Katika mchezo kati ya Italia dhidi ya Ufaransa kwa mara ya kwanza matumizi ya marudio ya video yalitumika rasmi na jambo ambalo Rais ya FIFA, Gianno Infantino ameliita, Historia kwenye mchezo wa Soka.
Video zilitumika pale ambapo Italia walilalamika kuwa walistahiki kupata penati kwa maana ya mchezaji Kurzawa kuwa amenawa mpira. Mwamuzi Bjorn Kuipers alisimamisha mchezo na marudio ya video kupitia televisheni maalumu yakafanyika na kupelekea maamuzi ya kutokutoa penalty.
Infantino ameelezea kuwa ana matarajio makubwa matumizi haya ya marudio ya video kuanza kutumika kwenye mashindano ya kombe la Dunia kule Urusi mwaka 2018.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG