Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania Mbwana Samatta anayecheza soka la kulipwa kwenye klabu ya Genk, Ubelgiji na kiungo wa kimataifa wa timu ya taifa ya Kenya na Tottenham ya Englnd, kwa pamoja wametuma salam za pole kwa wakazi wa Bukoba kutokana na janga la tetemeko la ardhi lililotokea hivi karibuni.
Wawili hao kwa nyakati tofauti kila mmoja ameandika ujumbe wa salam za pole kwa wakazi wa Bukoba waliopoteza ndugu jamaa na marafiki pamoja na hasara ya mali baada ya kukumbwa na tetemeko la ardhi.
“Poleni wakazi wa Bukoba kwa kupoteza ndugu pamoja na mali kutokana na tetemeko la ardhi, Mungu awatie nguvu na pia tuwaombee waliotangulia”, unasomeka ujumbe wa Samatta kwenye account yake ya twitter.
Kwa upande wa Wanyama, yeye aliandika ujumbe unaosomeka hivi: (tafsiri isiyo rasmi) “Mawazo na maombi yangu kwa watu wa Bukoba, Tanzania kufatia janga la tetemeko #TukoPamoja”, aliandika nyota huyo wa zamani wa Celtic na Southampton ambaye leo September 14 timu yake itashuka uwanjani kucheza mechi ya klabu bingwa Ulaya.
Tags
MICHEZO KIMATAIFA