Kila
siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za
Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account
yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza
kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.
Moja ya taarifa ambayo ipo kwenye magazeti ya leo ni pamoja na hii kutoka gazeti la Mtanzania lenye kichwa cha habari, ‘Kinyongo kinasababisha kansa’
Utafiti
uliofanywa nchini Marekani umebaini kuwa asilimia 61 ya magonjwa ya
saratani yanasababishwa na tabia za watu kushindwa kusamehe wenzao
waliowakosea.
Daktari
Michael Barry ndio aliofanya utafiti huo nchini humo, ambapo sasa
ameanzisha kliniki ya matibabu ya kusamehe Forgiveness Therapy.
Anasema
watu wengi hushindwa kuwasamehe wenzao, hali ambayo huwasababishia
msongo wa mawazo. ”wanakua hawana amani moyoni, muda mrefu wanakua na
msongo wa mawazo dhidi ya wale waliowakosea, mwisho hujikuta wakiugua
maradhi haya ya saratani.
Daktari
bingwa wa kutibu magonjwa ya akili na mihemko, Steven Standiford wa
Marekani anasema suala hilo lina ukweli ndani yake. ”wengi hushindwa
kuhimili hali ya kutosamehe lakini pasipo kujua kwamba hali hiyo kujiua
mwenyewe , kwani huwasababishia kupatwa kwa maradhi mbalimbali.
Akizungumza
na Mtanzania Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean
Road, Dk Julius Mwaiselage alisema anakubaliana na utafiti huo kwa kiasi
fulani.
Katika
utafiti wake , daktari huyo wa Marekani, Barry anaamini kupitia msamaha
lolote linawezekana. Katika kitabu chake kipya kiitwacho ‘The
Forgiveness Project’ (Mpango wa kusamehe) kinachoendelezea uvumbuzi wa
ajabu wa jinsi ya kupambana na ugonjwa wa saratani, kuwa na afya njema
na kuwa na amani. Dk. Barry anaelezea uchunguzi alioufanya juu ya
umuhimu wa msamaha katika afya na unavyoweza kuleta tiba ya ugonjwa
mkubwa kama saratani.
Source: MTANZANIA
Unaweza kupitia hapa habari nyingine kubwa kutoka kwenye magazeti ya Tanzania leo September 24 2106
Tags
UTAFITI