BANDA MEDIA BLOG

Aliyekuwa Waziri na Mwalimu Nyerere baraza la mawaziri 12 wa kwanza awataka vijana, kumuenzi Baba wa Taifa kwa kufanya kazi zenye matokeo

Balozi Mstaafu Job Lusinde akiongea kwenye Kumbukumbu ya miaka 17 tangu kifo cha hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere iliyofanyika katika viwanja vya Nyerere  mjini Dodoma

Aliyekuwa Waziri wa katika baraza la mawaziri la kwanza lililokuwa na mawaziri 12 Balozi Job Lusinde, Mkuu wa Wilaya  ya Dodoma Mjini Christina Mndeme, Madiwani na viongozi kadhaa wa CCM Wilaya wakishiriki zoezi la usafi katika viwanja vya sanamu ya Baba wa Taifa, wakati wa kumbukumbu ya Kifo chake kilichotokea miaka 17 iliyopita

Mmoja wa Vijana walioshiriki katika zoezi la usafi wakati wa kumbukumbu ya kifo cha hayati Baba wa Taifa uliofanyika katika viwanja vya Nyerere mjini Dodoma, akisafisha Sanamu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere IMETENGENEZWA NA BANDA BLOG

Wananchi mbalimbali wakishiriki katika zoezi hilo

Balozi Lusinde akizungumza na wakazi wa Dodoma wakati wa kumbukumbu ya kifo cha mwalimu Nyerere kilichotokea miaka 17 iliyopita

Mkuu wa Wiaya ya Dodoma Mjini Akishiriki kikamilifu katika zoezi la usafi  kwa kudeki katika maeneo ilipo sanamu ya Mwalimu Nyerere mjini humo

Balozi Job Lusinde, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Christina Mndeme na kaimu katibu wa CCM mkoa Salumu Kali wakipunga mikono wakati viongozi hao walipokuwa wakiongea na wakazi wa mji huo wakati wa kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa kilichotokea miaka 17 iliyopita 
NA JOHN BANDA, DODOMA
KUMBUKUMBU ya kifo cha Baba wa Taifa aliyefariki miaka 17 iliyopita imefanyika jana nchini kote ambapo kwa Dodoma, vijana  wametakiwa kuchapa kazi kama njia ya kumuenzi kwa vitendo hayati baba wa taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye alikuwa mwadilifu
mwenye upeo mkubwa na alitaka kila mtu achape kazi ili kuleta maendeleo.

Kauli hiyo ilitolewa jana na mwanasiasa mkongwe nchini balozi mstaafu
Job Lusinde wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya kumbukumbu ya
miaka 17 ya kifo cha baba wa taifa iliyofanyika katika viwanja vya
mwalimu Nyerere (Nyerere Square)Mkoani hapa.

Maadhimisho hayo yalienda sambamba na zoezi la kufanya usafi ikiwemo kuchangia Damu ambapo Aliwataka vijana kuacha kubweteka na kufanya kazi kwa bidii ili
kulikwamua taifa kwa kuzingatia maadili ya kazi na kuwatumikia
wananchi.

“Wakati wa Mwalimu watu walikuwa wakichapa kazi, hata  kwenye ofisi
habari za njoo kesho ilikuwa hakuna” alisema

“Wakati tunapata uhuru, ilikuwa uhuru na kazi, imani ya umoja ilikuwa
ikiongozwa kwenye nembo, leo tunashukuru baada ya uhuru na kazi sasa
ni hapa kazi tu” alisema

 Alisema mwalimu alikuwa akipenda kila mtu afanye kazi, alikuwa ni mtu
mwenye upeo mkubwa hakupenda makuu aliishi kama mtu wa kawaida na
hakupenda ufahari.
“Kama ulitaka kumuudhi mwalimu muoneshe ufahari, alikuwa mtu ambaye
hapendi makuu, tulijikuta tunafanya naye kazi vizuri kwa sababu
tulimuelewa” alisema
Alisema alikuwa akipenda watu wanaofanya kazi na kaamini kwa kuwapa
uongozi ili wamsaidie katika kazi za kulijenga taifa.
“Mimi nilipata uwaziri nikiwa na miaka 30, katika  baraza la kwanza la
mawaziri, lililokuwa na mawaziri 12 akiwemo Mwalimu Nyerere” alisema
Alisema kati ya hao 12 wamebaki yeye na Sir George Kahama huku 10 ambao kwa sasa ni marehemu ni Nsilo Swai, Oscar Kambona, Chief Fundikila, Paul Bomani, Sar Ernest Vace, Derick Braison, Amri Jamal, Tewa Said Tewa, Rashid Mfaume Kawawa na hayati Mwalimu Nyerere
“Tangu nimfahamu mwalimu mwaka 1948 nikiwa mwanafunzi Tabora Boys miaka mitatu baada ya vita kuu ya pili ya dunia alikuwa akiamini katika umoja ndani ya nchi na kati ya
mataifa mbalimbali, aliamini katika umoja wa Afrika na shirikisho la
Umoja wa Afrika” alisema

Alisema mwalimu aliendelea kuhubiri Umoja hadi alipofariki dunia
Pia alitaka watendaji na wananchi kuhakikisha mji wa Dodoma unakuwa
msafi ili kuweza kuendana na hadhi ya makao makuu ya nchi.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Christine Mndeme
alisema huu si wakati wa kulala bali kila moja achape kazi kwani hata
baba wa taifa alituhakikishia uhuru na kazi..
“Tumuenzi baba wa taifa kwa kujiepusha na mambo yasiyofaa, wengine
wanajiita panya road, wengine scorpion hatulitendei haki taifa hili”
alisema
Alisema serikali na jeshi liko imara katika kuhakikisha inakabiliana
na vitendo vyote vya kihalifu.
Pia aliwataka wananchi kutunza mazingira na akipatikana mtu anatupa
taka ovyo au kujisaidia ovyo faini yake ni Sh. 50,000 kwa kila kosa.
mwisho


Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG