Mkuu
wa kitengo cha mawasiliano Tanesco Leila Muhaji akizungumza na
waandishi wa kuhusu wizi wa vifaa vya umeme vyenye thamani ya milioni
61 vilivyokamatwa jijini Dar es salaam,Kulia ni Kaimu Kamishna wa Polisi
Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Lucas Mkondya.
Kaimu Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Lucas
Mkondya.(wa pili kushoto) akiwa na waandishi na walinzi wa Tanesco.
Kaimu Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Lucas Mkondya.(wa pili kushoto) akiwa na waandishi.
Kaimu Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Lucas Mkondya.(wa pili kushoto) akiwa na waandishi.
Gari la Tanesco likiwa na shehena ya vifaa vilivyokamatwa katika kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam.
Gari la Tanesco likiwa na shehena ya vifaa vilivyoibwa katika kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam.
Mwandishi Wetu.
Jeshi
la Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni likishirikiana na Kikosi kazi cha
kuzuia uharibifu wa miondo mbinu ya Shirika la umeme Tanzania Tanesco
Tarehe 18-10.2016 saa 10;00 jioni lilipata taarifa toka kwa raia mwema
kuwa katika maeneo ya Salasala huko Kinondoni jijini Dar es salaam kuna
watu wanaoiba na kuhuhujumu miundo mbinu ya Shirika hilo.
Kikosi
hicho kilifika eneo hilo katika nyumba ya Willfred Barutti (45) mkazi
wa Makumbusho na kufanya upekuzi kwenye nyumba hiyo ambapo walivipata
vifaa mbalimbali Line Meterial ambavyo hutumika kwa ajili ya kuunganisha
umeme mali ya shirika la Tanesco.
Polisi
walikwenda katika nyumba nyingine mali ya Betrice Emmanuel (42) mkazi
wa Salasala Mabanda wakafanya upekuzi na kufanikiwa kukamata vifaa
vifuatavyo;
Nyaya aina ya Drums’02,roller ya waya aina ya AICC ya umeme wa 50 mm ambazo hutumiwa na Tanesco kituo cha Kilimahewa huko Kawe Wilaya ya Kinondoni.
Thamani ya vifaa hivyo vinakadiliwa kuwa Tsh.61,000,000,Watuhumiwa wawili wanashikiliwa kwa mahojiano na Upelelezi utakapokamilika watapelekwa mahakamani kwa hatua za kisheria.

Tags
HABARI KITAIFA