Na Woinde Shizza,Arusha
Wito umetolewa kwa jamii ili waweze kuwa na maisha bora wawe na shughuli za halali
za kufanya zitakazo waingizia kipato,ili wasiwe tegemezi katika familia zao na jamii kwa ujumla.
za kufanya zitakazo waingizia kipato,ili wasiwe tegemezi katika familia zao na jamii kwa ujumla.
Kauli
hiyo imetolewa na Jaggy Singh ambaye ni mkurugenzi mkuu wa ushirika wa
Kimataifa wa wafanyabiashara Wakristo ( FGBMFI),ambapo amewataka watu
kufanya shughuli zao katika misingi iliyo halali ,katika uadilifu na
waepuke udanganyifu.
Singh
amesisitiza kuwa lengo kuu la mkutano ni kuwaleta wafanyabiashara
pamoja kubadilishana mawazo na changamoto wanazopitia,kuonyesha umuhimu
wa kuishi maisha ya uhalisia na kufanya kazi kwa bidii zaidi,ambapo
amewataka kuepuka udanganyifu wasiipige serikali chenga kwa kutokulipa
kodi ,wafuate utaratibu na sheria za nchi.
Kwa
upande wake raisi wa (FGBMFI) nchini Tanzania Injinia John Njau amesema
ushirika huo wa wafanyabiashara wa Kimataifa hawajishughulishi na
biashara peke yake bali wanahubiri Injili kamili kwa kutoa ushuhuda wa
vitendo hata kama wafanyabiashara wengine hawaamini lakini wao
wanatimiza
wajibu.
wajibu.
Ameainisha kuwa nchini Tanzania kwa sasa wana matawi ya ushirika huo wa wafanyabiashara Wakristo
yapatayo(7) ambayo ni kama ifuatavyo,
yapatayo(7) ambayo ni kama ifuatavyo,
Mbeya,Mwaza,Shinyanga,Kilimanjaro,Arusha,Dar
es-salaam,Manyara pamoja na Zanzibar ,na kwa upande wa Kimataifa kwa
ujumla yapo 169,ambapo kila tawi linafanya kazi kutokana na taaluma
walizo
nazo.
nazo.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mkutano huo John Majo
,ambaye pia ni mwenyekiti wa tawi la Arusha ,amesema kuwa ushirika huo
wa wafanyabiashara wa Kikristo mtu yeyote anaruhusiwa kujiunga maadamu
anajishughulisha ,awe ameajiriwa ,mfanyabiashara ,au mjasiriamali
anaruhusiwa nia yao kuu ni kuwaleta pamoja ili wamjue Mungu zaidi pia
“Unamkuta kijana yupo tu mtaani hataki kujishughulisha ukimtazama hana ulemavu wowote ,anapenda maisha ya kifahari na starehe lakini kazi hataki kufanya matokeo yake anajikuta amejiingiza kwenye mambo ya aibu na fedheha kubwa katika jamiii,inatuhuzunisha sana sisi kama wazazi badilikeni mjitume “alisisitiza
John.
Aidha
amewataka vijana wa kiume wasipende maisha ya urahisi bali wachape
kazi kwa bidii,wajitume waache tabia mbaya ya kuwa tegemezi kwani
wananguvu Mungu amewapa wazitumie ili kujiingizia kipato kwani
itawajengea heshima katika jamii
“Unamkuta kijana yupo tu mtaani hataki kujishughulisha ukimtazama hana ulemavu wowote ,anapenda maisha ya kifahari na starehe lakini kazi hataki kufanya matokeo yake anajikuta amejiingiza kwenye mambo ya aibu na fedheha kubwa katika jamiii,inatuhuzunisha sana sisi kama wazazi badilikeni mjitume “alisisitiza
John.
Katika
Kongamano hilo la Kimataifa la kila mwaka wasemaji walikuwa sita
,ambao waliongozwa na rais wa( FGBMFI )kutoka nchini Nigeria Injinia
,Ifeanyi .H.Odedo ambaye anasimamia matawi madogomadogo 3500 nchini
Nigeria
Tags
BIASHARA