Wanawake wanaofanya mapenzi mara kwa mara na wanaume tofauti wapo hatarini kuungua ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi ambapo 50 kati ya 1000 wanadhani kuwa na maambukizi hayo.
Naibu Waziri wa afya na ustawi wa jamii, Dokta Hamis Kigwangallah ametoa taarifa hiyo wakati anafungua mafunzo ya wanahabari wanawake wa mikoa ya Arusha, Manyara, Tanga na Kilimanjaro, yaliyoandaliwa na taasisi ya wanahabari ya Network for Development (NFD).Dokta Kigwangallah amesema kufanya ngono zembe mara kwa mara na wanaume tofauti, huwafanya wanawake kuwa hatarini zaidi kuungua saratani hiyo ya shingo ya kizazi; ambapo ugonjwa huo unaweza kupata tiba kama mgonjwa akibainika mapema na kupata matibabu.Kwa wastani kati ya wanawake 1000 wanawake 50 wanadhaniwa kuwa na ugonjwa huo na asilimia 37 wanaochelewa kupata tiba ufariki; hivyo amewataka waandishi wa habari wanawake, kupima afya zao na kwenda kutoa elimu juu ya ugonjwa huo.Dokta Kigwangallah amesema serikali imejipanga kuongeza uwezo wa kutoa tiba kwa kuongeza vituo vya tiba na uchunguzi kutoka kimoja cha ocean Road hadi vinne ambavyo ni ndani ya hospitali ya Bugando mkoani Mwanza, hospitali ya KCMC mkoani Kilimanjaro na hospitali ya rufani ya Mbeya.
Tags
AFYA
