Mahakama ya Wilaya Ilala jijini Dar es Salaam leo imemfutia shtaka la
unyang’anyi wa kutumia silaha, Salum Njwete maarufu kwa jina la
Scorpion baada ya upande wa mashtaka kuomba shtaka hilo liondolewe
mahakamani hapo kwa sababu hawana nia ya kuendelea na kesi hiyo.
Mtuhumiwa huyo ambaye ni mkazi wa Buguruni kwa Mnyamani anatuhumiwa
kumchoma visu na kisha kumtoboa macho, Said Ally mkazi wa Mabibo Hostel
hivi karibuni.