Kaimu
Meneja Mradi wa uboreshaji wa huduma za umeme jijini Dar es Salaam,
Mhandisi Iddi Rashidi, akizungumzia kukamilika kwa ujenzi wa mfumo wa
njia ya kusafirisha umeme ardhini, (Underground Transmission Lines),
kwenye shule ya sekondari ya wasichana Jangwani jijini Dar es Salaam,
Oktoba 22, 2016.
NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
SHIRIKA la umeme nchini
(TANESCO), limekamilisha ujenzi wa mfumo wa njia ya usafirishaji umeme
chini ya ardhi, (Underground Transmission Lines) , kutoka shule ya
sekondari ya wasichana ya Jangwani jijini Dar es Salaam na kutoka kituo
cha umeme cha Makumbusho kwenda kituo kipya cha kupozea umeme kilichoko
katikati ya jiji cha City Centre cha ukubwa wa 100MVA (2X50MVA),
132/33KV.
Akizungumzia maendeleo ya
utekelezaji wa mradi wa uboreshaji wa huduma za umeme jijini Dar es
Salaam, Kaimu Meneja wa Mradi huo, Mhandisi Iddi Rashidi, alisema,
kukamilika kwa ujenzi wa mfumo huo ambao utahusisha ujenzi wa mfumo wa
njia za usambazaji umeme chini ya ardhi (Underground Distribution
Lines), wa kilomita 4.3 wa msongo wa kilovolti 33 kwa ajili ya
kuunganisha kituo cha City Centre na vituo vingine vitatu vya Kariakoo,
Railway na Sokoine.
Akifafanua zaidi, Mhandisi Rashidi alisema, ujenzi wa mfumo wa njia ya usafirishaji umeme chini ya ardhi (Underground
Transmision Lines), kwa msongo wa Kv132 kutoka Makumbusho kwenda kituo
cha City Centre tayari umekamilika na ule wa kutoka shule ya sekondari
ya wasichana Jangwani kwenye City Centre pia umekamilika.
“Faida kubwa ambayo wakazi wa
jiji la Dar es Salaam watarajie ni kupata umeme wa uhakika (reliable
power supply ulio kwenye viwango stahiki, (Acceptable quality power
supply) hususan kwa wale wa maeneo ya katikati ya jiji,” Aliongeza
Meneja wa TANESCO Mkoa wa Ilala, Mhandisi Athanasius Nangali.
Akieleza zaidi, Mhandisi Nangai alisema, “Mradi huu unaviwezesha viituo tajwa kuwa na njia mbili za kuvvipatia umeme na hivyo kuwezesha kuwa na njia mbadala ya kupata umeme endapo njia moja kati ya hizo itakuwa na hitilafu.” Alifafanua.
Alisema kuongezeka kwa kituo cha
City Centre cha 100MVA, kunafanya jiji la Dar es Salaam pekee kuwa na
jumla ya vituo 9 vya aina hiyo. “Hivi sasa tunaweza kusema, ujenzi
umekamilika kwa zaidi ya asilimia 98, kinachoendelea ni kukamilisha
ujenzi wa mfumo wa njia ya kusafirisha umeme kupitia juu (Overhead
Transmission Lines), wa kilomita 1.3 wa msongo wa kilovolti 132 kutoka
kituo kikubwa cha kupozea umeme cha Ilala hadi shule ya sekondari ya
wasichana Jangwani ambapo utaungana na mfumo wa usafirishaji umeme chini
ya ardhi, (Underground Transmission Lines) kwenda kituo kikubwa cha
City Centre.” Alifafanua.
kutoka Makumbusho kwenda kituo
cha City Centre, umekamilikakatikati yan jiji utekelezaji wa Mradi huo,
unaofadhiliwa kwa pamoja na Serikali ya Tanzania na Finland, unahusisha
ujenzi wa kituo cha udhibiti mifumo ya usambazaji umeme (Distribution
SCADA System), katika msongo wa kilovolti 33 na 11.
“Tayari ujenzi wa kituo cha City Centre umekamilika kwa asilimia 100 na sasa tuko katika hatua za majaribio.” Alisema Mhandisi Rashidi.
Naye Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji, amewaomba wakazi wa jiji kuwa wavumilivu wakati zoezi
hili la kuboresha miundombinu likiendelea kwani huwa panatokea kukatika
kwa umeme sehemu Fulani Fulani ili kutoa nafasi kwa mafundi kufanya
kazi kwa usalama zaidi.
Meneja wa TANESCO Mkoa wa Ilala, Mhandisi Athanasius
Nangali, (kulia), akiwa na Kaimu Meneja Mradi, Mhandisi Iddi Rashidi
wakati wakizungumza na waandishi wa habari kuhusu mradi huo
Meneja wa TANESCO Mkoa wa Ilala, Mhandisi Athanasius
Nangali, (katikati), Kaimu Meneja Mradi, Mhandisi Iddi Rashid, (kulia),
Afisa Habari na Mawasiliano wa TANESCO, Hendry Kilasila, wakitembelea
eneo la ujenzi wa Mfumo huo shule ya sekondari Jangwani jijini Dar es
Salaam
Hizi ndio njia za kusafirisha umeme ardhini zilizojengwa kwenye shule ya sekondari ya wasichana Jangwani jijini Dar es Salaam
Nguzo
ya kusafirisha umeme wa juu kutoka Kituo cha Ilala kuja shule ya
sekondari ya wasichana Jangwani, ambapo zitaungana na Mfuko wa njia ya
kusafirisha umeme ardhini kupelekea katikati ya jiji
Mafundi wakiwa kazini
Mhandisi Nangali, (mbele), Kaimu Meneja Mradi, Mhandisi Rashid, (kulia), wakiangalia moja ya roller lenye nyaya.
Tags
HABARI KITAIFA









