BANDA MEDIA BLOG

JUMA KASEJA RASMI ASAINI MKATABA NA KAGERA SUGAR

kasejaggggggggggggggggggg

Na.Alex Mathias.

Klabu ya Kagera Sugar ya mkoani Kagera imetangaza rasmi kuingia mkataba na mlinda mlango wa zamani wa Simba,Yanga na Mbeya City,Juma Kaseka pamoja na mlinzi wa kati Mohamed Faki.

Akizungumza kwa njia ya simu Meneja wa timu hiyo Mohamed Hussein,amesema kuwa mapendekezo ya kocha Mexime yalikuwa sehemu tatu Mlinzi,mlinda mlango pamoja na mshambuliaji na tuweze kuwanasa hawa wawili bado tunatafuta mshambuliaji ambaye atakuja kutuletea faida katika kuwania nafasi ya ubingwa.

“Ni  kweli Kaseja tumemsajili hivyo tuna imani kuwa uzoefu wake katika michuano mbalimbali utakuwa msaada mkubwa katika kikosi chetu kwani ni golikipa mzuri bado hapa nchini japokuwa wanasema umri kuwa ni mkubwa na huu ni mwendelezo wa kuimarisha kikosi chetu kuelekea katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Tanzania bara’alisema Hussein

Aidha amesema kuwa msimu huu wanaamini kuwa watafanya vizuri kuliko msimu uliopita kwani kwenye mzunguko wa kwanza walimaliza wakiwa na pointi 9 tofauti na msimu huu wapo katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara.

Kagera Sugar ipo chini ya kocha wa zamani wa Mtibwa Sugar,Mecky Mexime na ameanza kukisuka upya kikosi hicho kutokana na kuwa na mapungufu katika sehemu mbalimbali  hasa kwenye ugolikipa ambapo Hussein Shariff ‘Cassillas’ameshindwa kuonesha kiwango kizuri huku akielaumiwa kuihujumu timu hiyo katika kipigo kikubwa cha magoli 6-3 toka kwa mabingwa watetezi Yanga.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG