Waziri wa Nchi Mhe. George B.Simbachawene (MB) akitoa hotuba kwa Baraza la Wafanyakazi lililofanyika katika Ukumbi wa Hazina ndogo mjini Dodoma ambapo amewataka kuongeza tija mahali pa kazi, kuwa na utendaji unaojali matokeo na kuepuka utendaji wa mazoea, Nidhamu na utendaji wa Watumishi wa Umma, kufanya mapitio yanayozingatia ubora katika utekelezaji wa majukumu kwa Ofisi ya Rais TAMISEMI kama taasisi na maadili kama nguzo muhimu ya kuepuka vitendo vya ubadhilifu na rushwa mahali pa kazi.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhandisi
Mussa Iyombe akifafanua jambo kuhusu utekelezaji wa maagizo ya Viongozi wa juu
na kuwatumikia wananchi kwa kupunguza changamoto zilizo katika Mamlaka za
Serikali za Mitaa, mara baada ya Waziri wa Nchi kushoto kwake Mhe. George
B.Simbachawene (MB) kutoa hotuba yake kwa Baraza la Wafanyakazi lililofanyika
katika Ukumbi wa Hazina ndogo mjini Dodoma
Waziri
wa Nchi Mhe. George
B.Simbachawene (MB) katika picha ya pamoja na
Wajumbe wanaounda Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais TAMISEMI na taasisi
zake DART, LAPF, Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo (LGTI) na Bodi ya Mikopo ya
Serikali za Mitaa waliokaa kulia kwake Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI
Mhandisi Mussa Iyombe , Mohamed Pawaga Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu
(DAHRM TAMISEMI), Susan Chekani Mkurugenzi wa Tawala za Mikoa TAMISEMI na
kushoto kwake ni Katibu wa Tawi la TUGHE TAMISEMI BW. Kepha Kupa, Mchenya
M.John Katibu wa TUGHE mkoa wa Dodoma na Bw. Akida mjumbe wa TUGHE kutoka Ofisi
ya Rais TAMISEMI
Na Fred Kibano
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene amewataka watumishi kufanya kazi kwa kufuata kanuni na taratibu za utumishi
na kuongeza tija mahali pa kazi na kujitathmini iwapo wamekidhi
matarajio ya Watanzania kwa kupata huduma bora.
Mhe. Simbachawene ameyasema
hayo wakati akitoa hotuba ya ufunguzi wa kikao cha Baraza la Wafanyakazi Ofisi
ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI) kilichofanyika katika
ukumbi wa hazina ndogo mjini Dodoma.
‘’kila mmoja anapaswa kutafakari haki zake na
zile anazopewa je zina usawa, kwani watumishi wengi wanadhani ni marupurupu ama
kuongezewa mshahara kwani ni zaidi
ya hayo ikiwemo namna anavyochukuliwa na
namna anavyo adhibiwa pale anapokosea na
kupewa pongezi pale wanapofanya vizuri’’ Alisema Mhe. Simbachawene
Pia Mhe. Simbachawene
amesema Wakuu wa kila Idara na Vitengo na watumishi wanapaswa kutatua tatizo la
ubinafsi kwani mfanyakazi anapofanya vizuri ni yeye ndiye anayepaswa kupewa
pongezi na siyo bosi wake kujiongezea mshahara, ‘’Sisi Viongozi tunapaswa
kutafakari mwisho wa siku tunafanya vizuri ama tunaumizana’’, Alisisitiza Mhe.
Simbachawene.
Vilevile, Mhe.
Simbachawene amesema kuna umuhimu wa kujua kila shilingi inayotumikaje na lazima
ionyeshe matokeo yake ni nini na kila robo mwaka ya Utekelezaji wa Bajeti kwani
kwa kufanya hivyo itawasaidia sana na kuongeza ufanisi wa kazi, ‘’ifike wakati tunafanya yanayopaswa
kufanywa,sisi ni watumishi wazuri ila tatizo linakuja kwenye utekelezaji kwani
dhana ya uwajibikaji wa Umma, nidhamu ya Utumishi wa Umma inapaswa iendelee kuimarika’’
Ameonya kuwepo kwa hali ya
rushwa hasa kutoka kwa walimu wanaohitaji kuhamia sehemu nyingine kwani kuna
watu wameanzisha vijiwe mitaani na
kutumia tovuti zisizo rasmi kwa kutapeli fedha
za walimu wanaohitaji huduma hiyo, hivyo basi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa inaendelea na uchunguzi na kwa wale watakaobainika hatua kali
zitachukuliwa dhidi yao.
Mhe. Simbachawene
alihitimisha kwa kusema ‘’kauli ya hapa kazi tu inapaswa kutekelezwa na
watumishi ili kufuata taratibu na kanuni za kikazi na jukumu la kusimamia
Serikali za mitaa na Halmashauri ni letu sote
kwani suala la maadili ni muhimu ili kuepuka vitendo vya rushwa.”
Tags
HABARI KITAIFA