Daktari bingwa wa upasuaji wa
ubongo na mishipa ya fahamu ambae pia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji
Taasisi ya MOI Othman Kiloloma akimueleza Waziri wa Afya Zanzibar
(hayupo pichani) jinsi Taasisi hiyo inavyookoa maisha ya watoto
wanaokabiliwa na maradhi hayo, (kulia) ni Afisa Habari wa GSM Foundation
Khalfani Kiwamba.
Waziri wa Afya Mahmoud Thabit
Kombo akizungumza na ujumbe wa Taasisi ya MOI na GSM Foundation ambao
wapo Zanzibar kuwafanyia upasuaji watoto wenye vichwa vikubwa katika
Hospitali ya Mnazi mmoja Mjini Zanzibar.
Dkt. Mohammed Ali Haji wa Kitengo
cha upasuaji vichwa maji na mgongo wazi wa Hospitali ya Mnazimmoja
akizungumzia ukubwa wa tatizo hilo katika visiwa vya Unguja na Pemba.
Dkt. Yassin Juma kutoka Kitengo
cha MOI akiwa katika maandalizi ya kumfanyia upasuaji wa kichwa mmoja ya
watoto waliofika Hospitali ya Mnazi mmoja kufanyiwa tiba hiyo.
Waziri wa Afya wa Zanzibar
Mahmoud Thabit Kombo wa nne (kulia) akiwa na Dkt. Othman Kiloloma watatu
(kulia)wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Wizara na maafisa
wa GSM Foundation.
Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.
Tags
AFYA