Mwenyekiti wa GFFD kt.
Christopher Elias akiongea na wadau pamoja na waandishi wa habari hawapo
pichani kuhusu ushiriki wao katika kuchangia maendeleo ya uzazi wa
mpango wakati wa kuhitimisha mkutano wa Bodi kwa nchizi lizoamua
kuongeza idadi ya watu wanaofahamu uzazi wa mpango kundi linalojulikana
kama “FP 2020 Reference Group uliofanyika jijini Dar es salaam katikati
ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy
Mwalimu.
Picha Na Ally Daud-MAELEZO.
………………………………………………………………..
Na Ally Daud-MAELEZO
Tanzania imepiga hatua kubwa
katika kuboresha huduma za uzazi wa mpango nchini tofauti na kipindi cha
nyuma ili kuweza kuondoa idadi ya ongezeko kubwa la watu na kupunguza
vifo kwa wajawazito na watoto kama sera ya Afya ya mwaka 2007
inavyosema.
Hayo yamesemwa na Waziri Ummy
Mwalimu(Mb) hivi karibuni wakati akifungua mkutano wa Bodi kwa nchi
zilizoamua kuongeza idadi ya watu wanaofahamu uzazi wa mpango kundi
linalojulikana kama “FP 2020 Reference Group.
“Tanzania imepiga hatua kubwa
katika kuboresha huduma za uzazi wa mpango nchini tofauti na kipindi cha
nyuma ili kuweza kuondoa idadi ya ongezeko kubwa la watu na kupunguza
vifo kwa wajawazito na watoto kama sera ya Afya yam waka 2007
inavyosema” alisema Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy amesema kuwa
mkutano huu unafanyika kwa mara ya kwanza barani Afrika na hususani
katika ardhi ya Tanzania hii ni kutokana na mafanikio makubwa
yaliyofikiwa katika eneo hili la uzazi wa mpango .
Waziri Ummy amesema kuwa
mafanikio hayo ni pamoja na ongezeko la bajeti katika eneo la uzazi wa
mpango na kupunguza hali utegemezi kwa kiasi kikubwa kutoka kwa
wahusani,kuimarisha mìfumo ya usambazaji wa dawa na vifaa tiba za uzazi
wa mpango hapa nchini
Mbali na hayo Waziri Ummy
alieleza kuwa katika mikoa ya kanda ya ziwa na magharibi mwa nchi
kumekuwa na ongezeko la uelewa na utumiaji wa huduma za uzazi wa mpango
kama vile mkoa wa Mara kuna ongezeko la utumiaji kutoka asilimia 10 hadi
asilimia 29 kuanzia mwaka 2010 hadi 2015 na katika mkoa wa kagera
kumekuwa na ongezeko kutoka asilimia 24 hadi asilimia 39.
Kwa upande wake Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia masuala ya uzazi
wa mpango Dkt.Babatunde alipongeza juhudi zinazofanywa na Serikali ya
nchi yetu katika kuhakikisha huduma hii inaimarika.
Mkutano huo wa siku tano ulioanza
Oktoba 31 hadi Novemba 4 mwaka huu unahudhuriwa na wajumbe na wadau
kutoka nchi mbalimbali duniani ikiwa na lengo la kujadili fursa
mbalimbali na changamoto zilizopo katika eneo la afya ya uzazi wa mpango
duniani.
Tags
AFYA