PICHA 2: Omog na Mingange Before and After Prisons vs Simba
byJohn Banda-
0
Kamera ya shaffihdauda.co.tzilifanikiwa
kuzinasa picha mbili za makocha Joseph Omog na Meja Mingange kabla na
baada (before and after) ya mchezo wa Tanzania Prisons na Simba
uliochezwa kwenye uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Kocha wa Simba Joseph Omog anaonekana mwenye furaha na amani kabla ya
kuanza kwa mchezo wakati anasalimiana na kocha wa Tanzania Prisons Meja
mstaafu Abdul Mingange. Kocha
wa Simba Joseph Omog (kuli) akiwa na tabasam na bashasha usoni wakati
akisalimiana na kocha wa Tanzania Prisons Meja mstaafu Abdul MingangeKocha
wa makipa wa Simba Adam Meja akisalimiana kwa furaha na kocha wa
Tanzania Prisons Abdul Mingange kabla ya mchezo wa Prisons vs Simba
Baada ya mchezo Omog anaonekana aliyepoteza furaha yake ya awali
baada ya kupoteza game ya pili mfululizo kwa kufungwa na Tanzania
Prisons. Kocha
wa Tanzania Prisons Meja Mingange (kushoto) na Joseph Omog wa Simba
wakitakiana kila la heri baada ya kumalizika kwa mchezo wao. Kocha wa
Simba anaonekana mwenye huzuni ukilinganisha na picha ya kwanza kabla ya
kuanza kwa mchezo