Diwani wa Kata ya Engutoto kwa
kupita Tiket ya Chadema Aman Reward alishirki katika uzinduzi wa Daraja
na kupongeza Viongozi wa Mkoa na Jiji kwa namna wanavyowatumika
wananchi
Diwani wa Kata ya jirani ya Themi
kupitia Tiketi ya Chadema Melance Kinabo pia alishirki katika uzinduzi
wa Daraja la Mto Kijenge.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Mrisho
Gambo(kwanza kulia) akipokea Kero kutoka kwa mwananchi kama
zilivyowasilishwa na Mama Debora wakati wa Unzinduzi wa Daraja la Mto
Kijenge
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Mrisho
Gambo akizungumza na wananchi wa Kata ya Engutoto na Moshono wakati wa
Uzinduzi wa Daraja la Mto Kijenge
Mkuu wa wa Mkoa wa Arusha Mhe.
Mrisho Gambo(kwanza kulia) akizungumza na wadau wa maendeleo Bw. Hans
Paul(pili kulia) na Bw. Jagjit Aggarwal
Daraja walilokuwa wanatumia
wananchi wa Engutoto na Moshono kabla ya kujengewa Daraja la kiwango na
Kampuni ya Dharam Sign Hanspaul
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo akizindua Daraja la Mto Kijenge
Hili ndilo Daraja lililojengwa na
wafadhili chini ya Bw. Hans Paul lina upana wa Mita 20, uwezo wa
kupitisha magari yenye uzito wa Tani 3, urefu kwenda juu Mita 2.2 na
uwezo wa kudumu kwa miaka 50.
………………………………………………………….
Nteghenjwa Hosseah – Arusha
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.
Mrisho Mashaka Gambo amezinduzaa daraja la Mto Kijenge linalounganisha
kata za Engutoto na Moshono ambalo limejengwa kwa ufadhili wa Kampuni ya
Dharam Singh Hanspaul.
Akizungumza katika uzinduzi huo
Mkuu wa Mkoa amesema daraja hilo ni ukombozi na msaada kwa wananchi
wengi ambao walikua wakipata adha kubwa ya kuvuka haswa wakati wa mvua
kutokana na kukosa kivuko cha uhakika na kivuko kilichokuwepo awali
kiliashiria hali ya hatari kubwa kwa watoto, wazee, waendesha pikipiki,
waenda kwa miguu wote na zaidi hakuna Gari lililokuwa na uwezo wa
kupita hapo.
Hii ndio tunayoita kurudisha kwa
jamii “Community Social Responsibility”, kampuni hii ya Hanspaul imetoa
msaada ambao utatoa mchango mkubwa sana kwa jamii na sisi kama Serikali
tunafarijika kwa kuona wadau wanaunga mkono jitihada za Serikaili kwa
kiwango hiki hili ni jambo la kuigwa na Kampuni nyingine wajifunze
katika hili.
Katika uzinduzi wa daraja hili Rc
Gambo alitumia fursa hiyo alisikiliza kero za wananchi waliohudhuria na
ambao wamelalamikia uuzaji holela wa maeneo ya wazi ya Serikali hali
inayopelekea uhaba wa maeneo ya kujenga huduma za kijamii kama zahanati
na shule huduma ambazo hazipatikani katika kata ya Engutoto hiyo hivyo
wameiomba serikali itatue tatizo hilo ili wananchi wapate huduma bora za
ijamii.
Akiwasilisha kero zake mbele ya
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bi. Zaituni Marunda amesema kuwa licha ya uuzaji
holela wa ardhi kuna migogoro ya ardhi katika kata hiyo na wananchi
wengi wanaomiliki ardhi bado hajapatiwa hati jambo ambalo linawapa
wasiwasi kuwa huenda ardhi zao zikamegwa na wawekezaji.
Aidha Neema John aliongeza kuwa
kwa kipindi kirefu katika maeneo hayo wamekuwa wakisumbuliwa na kero za
maji, umeme na Zahanati hivyo wameiomba Serikali iwasaidie kutatua kero
hizo znazowaathiri zaidi kinamama ambao hutembea umbali mrefu wakitafuta
huduma za maji pamoja na kupata taabu wakati wa kujifungua.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho
Gambo ameagiza ofisi ya Mkurugenzi kumkabidhi ripoti ya maeneo ya wazi
ya jiji yaliyouzwa kienyeji ili aweze kushughulikia kero na pia aliweza
kuhamasisha ujenzi wa Zahanati ya Kata kwa kuchangia Bati 100 na
kuungwa mkono na Bw. Hans Paul aliyetoa matofali 5000 huku Bw. Jagjit
Aggarwal akichangia mifuko ya saruji 200 na Mkurugenzi wa Jiji Bw.
Athumani Kihamia kuahudi kukamilisha ujenzi wa zahanati hiyo.
Daraja la Mto kijenge lilioanza
kujengwa mwezi Juni na kukamilika Agost 2016 lina upana wa Mita 20,
uwezo wa kupitisha magari yenye uzito wa Tani tatu(3), urefu kwenda
juu ni mita 2.2, uimara wa pekee na linaweza kudumu kwa miaka 50;
Ujenzi wake umegharimu kiasi cha shilingi milioni 67 .
Tags
MIUNDOMBINU