Wanawake wakutana kutathimini mwaka mmoja wa Serikali ya Rais Magufuli
byJohn Banda-
0
Mwenyekiti
wa Mfuko wa Wanawake Tanzania, Profesa Ruth Meena (katikati) akisoma
tamko la wanawake kwa wanahabari kuelezea tathini ya mwaka mmoja wa
Serikali ya awamu ya tano mara baada ya kufunguliwa kwa mkutano huo.
Wengine ni viongozi na wajumbe wa mkutano huo.Mwenyekiti
wa Mfuko wa Wanawake Tanzania, Profesa Ruth Meena (wa pili kushoto)
akisoma tamko la wanawake kwa wanahabari kuelezea tathini ya mwaka mmoja
wa Serikali ya awamu ya tano mara baada ya kufunguliwa kwa mkutano huo.
Wengine ni viongozi na wajumbe wa mkutano huo.Aliyekuwa
mgombea nafasi ya urais wa Chama cha ACT – Wazalendo, Anna Mghwira
(kulia) ambye pia ni Mwenyekiti wa chama hicho taifa akichangia mada
katika mkutano wa wanawake ulioandaliwa na Mfuko wa Wanawake Tanzania.Baadhi
ya washiriki katika mkutano huo wakijadiliana masuala anuai. Mkutano
huo ulioshirikisha wanawake kutoka mikoa mbalimbali umefanyika katika
Ukumbi wa Mikutano wa Mtandao wa Jinsia Tanzania, TGNP Mabibo jijini Dar
es Salaam.Mkurugenzi Mtendaji wa WFT, Mary Rusimbi (kushoto) akichangia mada katika mkutano huo.Baadhi
ya wajumbe washiriki wa Mkutano wa Wanawake ulioratibiwa na Mfuko wa
Wanawake Tanzania, wakizungumza kuchangia mada mbalimbali zilizotolewa
katika mkutano huo. Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa
Mtandao wa Jinsia Tanzania, TGNP Mabibo jijini Dar es Salaam.Baadhi
ya washiriki katika mkutano huo wakiserebuka na nyimbo za wanawake.
Mkutano huo ulioshirikisha wanawake kutoka mikoa mbalimbali umefanyika
katika Ukumbi wa Mikutano wa Mtandao wa Jinsia Tanzania, TGNP Mabibo
jijini Dar es Salaam.WANAWAKE kupitia Mfuko wa Wanawake Tanzania wamekutaka katika
mkutano na kutoa tathimini ya mwaka mmoja wa Serikali ya Awamu ya Tano
inayoongozwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli. Mkutano huo ulioshirikisha
wanawake kutoka mikoa mbalimbali umefanyika katika Ukumbi wa Mikutano
wa Mtandao wa Jinsia Tanzania, TGNP Mabibo jijini Dar es Salaam. Akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa mfuko huo,
Profesa Ruth Meena aliipongeza Serikali ya Dk. Magufuli kwa mafanikio
ilioanza kuonesha katika ukusanyaji na usimamizi wa mapato pamoja na
mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa huku akiiomba Serikali kutambua
pia kwa vitendo mchango wa wanawake katika ujenzi na maendeleo ya
nchini. Baadhi
ya wajumbe washiriki wa Mkutano wa Wanawake ulioratibiwa na Mfuko wa
Wanawake Tanzania, wakizungumza kuchangia mada mbalimbali zilizotolewa
katika mkutano huo. Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa
Mtandao wa Jinsia Tanzania, TGNP Mabibo jijini Dar es Salaam.Baadhi
ya wajumbe washiriki wa Mkutano wa Wanawake ulioratibiwa na Mfuko wa
Wanawake Tanzania, wakizungumza kuchangia mada mbalimbali zilizotolewa
katika mkutano huo. Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa
Mtandao wa Jinsia Tanzania, TGNP Mabibo jijini Dar es Salaam.Alisema wanawake nchini watafurahia kuona Serikali ya Rais
Magufuli inakisikia kilio cha wanawake juu ya vitendo vya udhalilishwaji
katika mitandao ya kijamii, ikiwemo kuonesha uwajibikaji katika
kushughulikia sheria kandamizi ambazo bado zinaibana jamii hiyo. “…Tunaiomba Serikali ikemee suala la udhalilishaji wa
wanawake katika mitandao ya kijamii, Sheria ziwekwe kuwalinda wanawake.
Imefanya vyema kupiga marufuku nyimbo mbili na ngoma zinazikwenda
kinyume na maadili yetu hivyo ikemee pia pale wanawake
wanapodhalilishwa,” alisema Profesa Meena. Aidha mkutano huo ulipongeza mfumo wa elimu bure unaotolewa
sasa na Serikali kwa kuwa unatoa fursa kwa familia maskini hasa za
wanawake wajane kupata elimu jambo ambalo awali lilikuwa changamoto kwa
jamii hiyo. Walipongeza pia uwajibikaji unaoendelea kusimamiwa na
Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Magufuli umeongeza nidhamu
kazini pamoja na kuwajibika katika utoaji huduma. Mkutano huo ulishirikisha wanawake wanaharakati ngazi za
jamii kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Visiwani ambapo
walijadili masuala mbalimbali ikiwemo kushirikishana changamoto kutoka
maeneo yalikotoka wajumbe wa mkutano na kuangalia mbalengo ya baadae. Baadhi
ya wajumbe washiriki wa Mkutano wa Wanawake ulioratibiwa na Mfuko wa
Wanawake Tanzania, wakizungumza kuchangia mada mbalimbali zilizotolewa
katika mkutano huo. Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa
Mtandao wa Jinsia Tanzania, TGNP Mabibo jijini Dar es Salaam.Baadhi
ya wajumbe washiriki wa Mkutano wa Wanawake ulioratibiwa na Mfuko wa
Wanawake Tanzania, wakizungumza kuchangia mada mbalimbali zilizotolewa
katika mkutano huo. Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa
Mtandao wa Jinsia Tanzania, TGNP Mabibo jijini Dar es Salaam.