BANDA MEDIA BLOG

SIKU YA WALEMAVU DUNIANI SASA KUSHEHEREKEWA KATIKA MIKOANI


Tokeo la picha la waziri simbachaweneNa Shani Amanzi 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali  za Mitaa [TAMISEMI] George SimbaChawene amewagiza Wakuu wa Mikoa   nchini kuhakikisha maadhimisho ya siku ya walemavu yanayoanzimishwa Duniani kote yanafanyika katika mikoa yao badala ya kukusanyika  jijini Dar-es-salaam


Akiongea kwa niaba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri Simbachawene amesema tamko hilo lilitokana na ombi la Chama Cha Walemavu  kuomba halmshauri za wilaya ziwasafirishe wanachama wa vyama vya walemavu ili wafanye maadhimisho hayo kitaifa jijini Dar-es-salaam Desemba3,2016


‘’kwa hiyo nichukue nafasi hii kuwaagiza wakuu wa mikoa na halmashauri  kuhakikisha wanatoa ushirikiano  wa kutosha kwa vyama vya walemavu ili viweze kufanikisha maadhimisho hayo” Alisisitiza Simbachawene.

Simbachawene ametoa agizo kwa mkoa wa Dar-es-salaam kufanikisha sherehe hizo katika halmashauri zake zote, “Mkuu wa Mkoa Paul Makonda anapaswa kuchukua hatua   kwa kushirikiana na halmashauri zote za Dar-es-salaam, ahakikishe maadhimisho hayo yanafanikiwa kwa kuwapa msaada wote unaostahili” 

Vilevile amesema, “kwa kufanya hivyo hii itasaidia kupunguza gharama badala ya walemavu wa vyama hivyo wote wangetoka kwenye wilaya zetu kuja Dar-es-salaam, sasa shughuli hizo zifanyike maeneo ya  mikoa yao na wilaya zao na  natoa maelekezo hayo kwa sababu muda wa kufanya maadhimisho hayo  ni mchache  na  kuanzia leo nimeamua  kutumia  njia hii ili tuweze kuwasiliana kwa haraka.” alisema

Aidha Simbachawene ametoa pongezi  kwa vyama vyote vya walemavu nchini kwa namna wanavyoshirikiana na kutoa maoni yao kwa  Serikali, lakini pia Serikali ipo pamoja nao na wataendelea kushirikiana nao kuweka mbele maslahi yao,  kutatua matatizo yao na katika hili shughuli ya kuadhimisha siku ya walemavu duniani Serikali ipo pamoja nao .

  

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG