Wakati
Rais Magufuli akitimiza mwaka mmoja tangu aingie madarakani Leo
November 04 2016 amekutana na waandishi wa habari IKULU Dar es salaam
na kujibu maswali mbalimbali, moja ya swali, lililoanza kuulizwa
lilimtaka Rais Magufuli kusema namna anavyojitathmini katika mwaka wake
mmoja wa uongozi. Rais Magufuli amejibu…
>>>Umeniuliza
swali gumu, ni vizuri watu kukutathmini kuliko kuliko wewe mwenyewe
kujitathimini, nilipokuwa nimechaguliwa yapo tuliyokuwa tumeyaahidi,
nilitoa hotuba ya kwanza bungeni nilisema nataka kuwa na serikali ya
hapa kazi tu, kila mtu afanye kazi, nahisi nimetimiza hayo
Tags
HABARI KITAIFA