Afisa wa jeshi la polisi kitengo cha Usalama ,Haji
Nduya akitoa mafunzo ya usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule ya
msingi Oysterbay jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya
wiki ya nenda kwa usalama kanda maalum ya Dar es Salaam chini ya
udhamini wa TBL Group, ikiwa mkakati wa n kupunguza ajali za barabarani.
Mkaguzi
msaidizi wa Jeshi la polisi kitengo cha Usalama barabarani kutoka makao
makuu ya Jeshi hilo ,Erick ndidi (kulia) na Afisa wa Masuala Endelevu wa TBL Group Irene Mutiganzi (kushoto)wakitoa mafunzo ya usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule ya masingi ya Oysterbay jijini Dar es Salaam
Afisa masuala endelevu wa TBL Group Irene Mutiganzi (kulia) akifafanua jambo kuhusiana na usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule ya msingi ya Oysterbay jijini ya Dar es salaam wakati wa mafunzo ya usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule hiyo.
Wanafunzi wa darasa la kwanza shule ya msingi ya Oysterbay jijini Dar es salaam wakionyeshwa alama za barabarani na Afisa maswala endelevu wa TBL Group Irene Mutiganzi (kushoto) wakati wa mafunzo hayo.
Mkaguzi msaidizi wa Jeshi la polisi kitengo cha Usalama barabarani kutoka makao makuu ya Jeshi hilo ,Erick ndidi akiowaongoza wanafunzi wa
shule ya masingi ya Oysterbay jijini Dar es Salaam, kuvuka barabara ya
Haile Selassie, kwa kutumia alama za barabarani (zebra). 
Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la polisi kitengo cha Usalama barabarani kutoka makao makuu ya Jeshi hilo ,Erickdidi akiongozana na wanafunzi wa shule ya masingi ya Oysterbay jijini Dar es Salaam, kuvuka barabara ya Haile Selassie, kwa
kuongozwa na mwanafunzi wa shule hiyo Jesca John (kushoto) wakati wa
maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani Kanda maalum ya Dar
es Salaam,yaliyodhaminiwa na TBL Group ikiwa ni sehemu ya kupunguza
ajali kwa watoto wa shule wakati wanapovuka barabara wakienda au kutoka
shuleni.
…………………………………………………………..
Yamedhaminiwa na TBL
Katika
maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani mkoani Dar es
Salaam,mwishoni mwa wiki Jeshi la Polisi Kanda ya mkoa wa Kinondoni
liliendesha mafunzo ya usalama barabarani katika shule ya msingi
Oysterbay chini ya udhamini wa kampuni ya TBL Group.
Wakati
wa mafunzo hayo yaliyoendeshwa na askari kutoka Jeshi la Polisi kikosi
cha Usalama barabarani wanafunzi waliweza kufundishwa alama mbalimbali za bararani,mambo ya kuzingatia wanapokuwa barabarani na jinsi ya kuvuka barabara kwa tahadhari.
Pia wanafunzi walipata fursa ya kuuliza maswali mbalimbali kuhusiana na masuala ya usalama barabarani na waliulizwa maswali ya chemsha bongo kuhusiana na elimu ya mafunzo waliyopatiwa.
Afisa mawasiliano wa TBL Group,Amanda Walter, alisema kuwa TBL imedhamini mafunzo haya ikiwa ni mwendelezo wake wa kuunga mkono jitihada za serikali za kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kampeni za usalama barabarani.
“Kampuni ya TBL tunao
mkakati wa kuendelea kushirikiana na serikali kupitia kikosi cha Polisi
wa Usalama barabarani na wadau wengine kuhakikisha tunapunguza matukio
ya ajali za barabarani nchini ambazo zimekuwa zikisababisha vifo,ulemavu
na hasara kwenye jamii”.Alisema.
Alisema mpango wa kuwafikishia wanafunzi wa shule za msingi elimu ya usalama barabarani hauna budi kuungwa mkono kwa nguvu zote kwa kuwa wakielewa tatizo hili mapema itakuwa ni rahisi kutokomeza tatizo hili katika siku za usoni. “Wanafunzi
wana uelewa mkubwa na ni rahisi kushika wanayofundishwa pia wanaishi
katika mazingira ambayo ni muhimu kuwa na ufahamu wa masuala haya”.
Mbali
na kudhamini mafunzo haya ya wanafunzi kampuni ya TBL Group imekuwa
mmoja wa wadhamini wakuu wa Wiki ya Nenda Kwa Usalama ngazi ya kitaifa
ambapo ilitoa vifaa mbalimbali vya uhamasishaji ikiwemo gari maalumu ya
kupimwa afya za madereva la Zahanati inayotembea maarufu kama ‘Zahanati
Mwendo’,huduma ambayo ni ya kwanza nay a aina yake nchini ambayo mpaka sasa inaendelea kuchangamkiwa na madereva popote linapopita gari hilo.
Tags
ELIMU