BANDA MEDIA BLOG

Waziri Nape Nnauye ampongeza Rais wa Chama cha Riadha Tanzania (RT) Ndugu Anthony Mtaka

mtakati
Rais wa Chama cha Riadha Tanzania (RT) Ndugu Anthony Mtaka.
………………………………………………………………………….
Mhe. Nape Mosses Nnauye, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo anapenda kutuma salamu za pongezi kwa Rais wa Chama cha Riadha Tanzania (RT) Ndugu Anthony Mtaka kwa kuaminiwa kwa mara nyingine na wanachama na kukabidhiwa jukumu hili la kuwaongoza kwa muhula mwingine wa miaka minne. Aidha, anawapongeza viongozi wengine waliochaguliwa.

Pongezi za dhati ziwafikie viongozi wote wa uongozi uliopita kwa moyo wao wa uzalendo waliouonesha kwa kufuata katiba ya Chama cha Riadha Tanzania, kuachia madaraka na kupisha uchaguzi kama katiba inavyoelekeza.
Mheshimwa Waziri anawapongeza wanachama wote wa  Chama cha Riadha Tanzania (RT) kwa uvumilivu na subira waliyoionesha wakati wa uchaguzi huu ambao uliendeshwa kwa amani na utulivu na hatimaye kuwapata viongozi wapya na kamati tendaji ya Chama cha Riadha Tanzania (RT).
Aidha Waziri Nape anapenda kuviasa vyama vyote vya michezo nchini kufuata katiba za vyama vyao na kuepuka kung’ang’ania madaraka ili kudumisha utawala bora katika michezo.
Ninawatakia uongozi mpya utendaji mwema wa Majukumu yao pia ninawaasa wafuate taratibu za uongozi kama zinavyo ainishwa katika sheria za nchi na katiba na sheria za uongozi  ndani ya  Chama cha Riadha Tanzania (RT).
Imetolewa na Waziri Wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG