BANDA MEDIA BLOG

AFRICAN LYON YATAMBA KUIMALIZA YANGA MCHEZO WA LIGI KUU


african-lyon_1fjazl6tsg3fz1jct4c4e7zl5d
Na.Alex Mathias
Uongozi wa timu ya soka ya Afrika Lyon ya jijini Dar es salaam,umesema kwamba kikosi chao kinaendelea vyema kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wao wa ligi kuu ya Tanzania bara unaotaraji kuchezwa siku ya ijumaa kwenye uwanja wa Uhuru dhidi ya Young Africans.

Mkurugenzi wa ufundi wa timu hiyo Charles Otieno amesema kwamba kwa upande wao msimu huu wamejipanga kufanya vizuri kwa mechi zote,kwani nia yao ni kupata pointi tatu ili kujiweka kwenye mazingira mazuri katika msimamo wa ligi.
Otieno amesema kwamba wanafahamu kuwa Yanga ni wazuri,lakini hilo haliwapi hofu yeyote kwani kikosi chao kimejiandaa kikamilifu kuhakikisha kuwa wanapata alama tatu muhimu.
Lyon mechi yake ya mzunguko wa pili waliweza kuwabana mbavu matajiri wa jiji la Dar es salaam Azam FC kwenye uwanja wa Uhuru na mzunguko wa pili waliweza kufungwa jumla ya magoli 3-0 na Yanga hivyo wamejipanga kuwashushia kipigo wanajangwani hao.
Kwa upande wa Yanga wao walianza vema katika mzunguko wa pili baada ya kupata ushindi wa magoli 3-0 toka kwa wanajeshi JKT Ruvu Stars na wakiwa na benchi la ufundi jipya likiongozwa na kocha Mkuu George Lwandamina na ikumbuke Lyon ndio timu ya kwanza kuvunja mwiko wa Simba wakutofungwa baada ya wekundu hao kulala kwa goli 1-0 dakika ya za lala salama.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG