BANDA MEDIA BLOG

SIMBA YAINGIA MKATABA NA KOCHA TOKA KENYA


idd-1
Klabu ya Simba imeingia mkataba wa mwaka mmoja na kocha wa makipa Iddi Salim Raia wa Kenya ikiwa ni mara yake ya pili kuinoa Simba.
Kocha huyu mwenye uzoefu katika kazi yake alitumbuliwa na Simba akiwa pamoja na kocha wa kipindi kile Mwingereza Dylan Kerr baada ya kufanya vibaya hivyo wote walitupiwa virago.
Safari hii amerejea Simba akiwa amejifua zaidi na kupata leseni ya Shirikisho la Soka Ulaya (Uefa), maana yake anaweza kufanya kazi nchini humo.
Kocha huyu pia alishawahi kufanya kazi na Mabingwa wa Zamani wa Kenya timu ya Gor Mahia, AFC Leopards za Kenya pamoja na timu ya taifa ya nchini hiyo, Harambee Stars.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG