BANDA MEDIA BLOG

BONDIA MESHACK MWANKEMWA AWASILI DAR KUMKABILI RAMA SHAURI


boa
Mabondia Mesharck Mwankemwa wa Mbeya na Mbwana Matumla wakioneshana ubabe makonde wakati wa mazoezi kabla ya mpambano wao  Feb. 5 / 2017 utakayofanyika katika ukumbi wa uwanja wa ndani wa Taifa Mwankemwa atapanda ulingoni na Ramadhani Shauri na Matumla atamkabili Seleiman Shabani Picha na SUPER D BOXING NEWS
………………………………………………………………………………
Na Mwandishi Wetu
Bondia Meshack Mwankemwa wa Mbeya ameingia jijini Dar es salaam kwa ajili ya mpambano wake na Ramadhani Shauri mpambano utakaokuwa wa raundi kumi za ubingwa wa EAST/ CENTRAL AFRICA siku ya Feb 5/ 2017 katika uwanja wa ndani wa Taifa .
Akizungumza na wahandishi wa habari Promota wa mpambano huo Sadick Kinyogoli amesema kuwa huu ni wakati wa mwisho wa kuelekea mpambano wenyewe  utakaofanyika mwishoni mwa wiki hii kwenye uwanjwa ndani wa Taifa.
Sadick Kinyogoli amesema  Mwankemwa ametua jijini tangu mwishoni mwa wiki iliyopita na Shauri ni mkazi wa jiji la Dar es salaam kwa  hiyo mpambano huo  utakuwa mkali sana kwa kuwa mabondia wote wameshacheza mapambano makubwa ya kimataifa hivyo wapenzi wajiandae na kufika  mapema ili kuangalia burudani ya mchezo wa masumbwi waliyoikosa kwa kipindi kirefu.
Katika mpambano huo pia kutakuwa na mapambano mengine ya kusindikiza mtanange huo ambapo Kinyogoli  ameongeza  kuwa bondia Mohamed Matu, atapambana na Mfaume Mfaume wakati bondia chipukizi anayekuja kwa kasi katika mchezo huu wa masumbwi Iddi Mkwela ataonyeshana umwamba na Manyi Issa mpambano  ambao utakuwa na  raundi kumi zisizokuwa na ubingwa
Mchezo mwingine wa ubingwa wa taifa utakuwa kati ya Said Chino na Twalib Tuwa ubingwa wa taifa wa TPBC mkanda ambao unatetewa na Tuwa  Husein Pendeza wa Ashanti Boxing Clab ya Ilala yeye atavaana na Said Hamdani kutoka Mbezi Conetion na Mbwana Matumla atazichapa na Suleimani Shabani
Pamoja na mpambano hayo kutakuwa na mpambano  mwingine wa kimataifa kwa akina dada Anisha Bashir kutoka Malawi na Ester Boazi Kazeba wa Tanzania
Kinyogoli ameongeza kwa kusema kuwa mabondia wote watapima uzito pamoja na Afya zao siku ya Feb. 4/ 2017 katika hotel ya Atrium iliyopo Sinza Afrika Sana hivyo mabondia wote w

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG