WATU 15 waliofukiwa kwa kifusi katika mgodi wa dhahabu wa Kampuni ya RZ
Union Mining Ltd uliopo Kata ya Nyarugusu mkoani Geita, wameokolewa wote
wakiwa hai kutokana na jitihada zilizofanywa na wataalamu wa mgodi huo
na mingine kwa kushirikiana na serikali.
Habari zilizotufikia punde ni kwamba watu hao wameokolewa baada ya
kukaa takribani siku tatu ndani ya mgodi bila kupata chakula na bila
kuona mwanga wa jua.
Aidha, taarifa za awali zinasema kuwa baada ya kuokolewa watu hao wamewekwa chini ya uangalizi wa
karibu na wataalamu wanaendelea na uchunguzi huo ambapo baada ya muda itatolewa ripoti kamili.
Tags
HABARI KITAIFA



