Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Taifa,
Freeman Mbowe amesema kuwa kitendo cha kumkata Waziri Mkuu wa zamani,
Edward Lowassa mkoani Geita kimedhihirisha polisi kutumika na Chama Cha
Mapinduzi wakati wa chaguzi mbalimbali.
Mwenyekiti huyo alisema jeshi la polisi limekuwa likiwakamata na
kuwaweka ndani viongozi mbalimbali wa chama chake kwa shinikizo la CCM
na kuwataka Watanzania kulaani ukamataji huo kwa kuwa ni uhuni wa
kisiasa.
Mbowe ametoa kauli hiyo leo jijini hapa wakati akifungua Kikao cha
Kamati Kuu ya chama hicho kilichohudhuriwa na wajumbe mbalimbali akiwemo
Lowassa pamoja na baadhi ya wabunge.
Tags
SIASA
