MBUNGE
wa Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa ,mwenye kofia aina ya pama akionekana
pichani akisaidiana na ndugu wa mgonjwa kumbeba kwenye kitanda kumpeleka
wodini, baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika kituo cha afya cha
Mlandizi.(Picha na Mwamvua Mwinyi)
Mbunge
wa Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa akiwakabidhi zawadi ya maboksi ya
vyombo vya jikoni watumishi wote katika kituo cha afya cha Mlandizi
kama motisha na kuendelea kuwatia moyo kuwahudumia kiafya wananchi wa
jimbo hilo .(Picha na Mwamvua Mwinyi)
……………………………………………………………………
Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha Vijijini
MBUNGE
wa jimbo la Kibaha Vijijini ,Hamoud Jumaa,amefanya ziara ya kushtukiza
katika kituo cha afya Mlandizi na kuvumbua madudu ikiwemo baadhi ya
wauguzi kwenye wodi ya uzazi kutoa lugha chafu kwa wagonjwa.
Aidha
katika ziara hiyo amekutana na malalamiko juu ya wauguzi wanafunzi
wanaokwenda kufanya mafunzo kwa vitendo kituoni hapo,ambao wamekuwa
wakitoa siri za maumbile ya akinamama wanaokwenda kujifungua nje ya
kituo.
Kufuatia
hali hiyo,Jumaa alimuasa mganga mfawidhi kituo cha afya Mlandizi na
mganga mkuu halmashauri ya wilaya ya Kibaha,kuwachukulia hatua watumishi
wazembe na wanatoa lugha chafu kwa wagonjwa .
Alisema
amepokea pia malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kuhusiana na wakunga
na wauguzi katika wodi ya uzazi kutokuwa na lugha rafiki kwa akinamama
wanaokwenda kujifungua.
Hata hivyo akiwa katika ziara hiyo alikuta vitanda vya wagonjwa katika wodi ya uzazi vikiwa havijatandikwa mashuka .
Mbali
ya hilo mara baada ya kufika kituo cha afya Mlandizi,Jumaa alimkuta
mama mmoja aliyejifungua watoto mapacha ambapo mtoto mmoja alifariki
akiwa Tumbi kutokana na tatizo lililoshindwa kuzuilika :”na kufikishwa
ktuoni hapo kutokana na kuugua akitokea nyumbani huku hana msaada wa
kupelekwa wodini.
Mbunge
huyo alimuuliza muuguzi aliyemkuta akibishana na ndugu wa mgonjwa na
kisha kuamua kumbeba mama huyo pamoja na ndugu yake hadi wodini na
aliendelea na matibabu.
Jumaa
alisema baadhi ya wauguzi katika wodi hiyo na watumishi wamekuwa na
dharau na maneno machafu kwa wagonjwa hali inayosababisha wananchi
kukata tamaa yakufuata huduma kituoni hapo.
“Mimi
mwenyewe nilikuja hapa saa 7 ya usiku na kwenda mapokezi ambako
nilikutana na wadada wawili ,mmoja alinipokea vizuri lakini mwingine
alinijibu maneno makali huku akiwa hajajua mimi ni nani”
“Vitendo
hivi havipendezi kwa wagonjwa hata kwa ndugu zao wanaowauguza ,kuweni
wakarimu ,toeni huduma bora na upendo”alifafanua Jumaa.
Aliwaomba
watumishi na wahudumu hao kutimiza wajibu wao pasipo kuwanyanyasa
akinamama hao kwani wanapofanya uzembe na manyanyaso ni chanzo cha vifo
vya uzazi na watoto .
“Unakuta mtumishi ama mhudumu wa afya katika wodi ya uzazi anasuka ama wanapiga soga wakati kuna mama analalamika maumivu,wana wajibu maneno machafu, kiukweli watumishi wa aina hii lazima wawajibishwe”alisema Jumaa.
Katika hatua nyingine alikuta vitanda vya kupimia wagonjwa na magodoro ambayo yalipelekewa kituoni hapo kama msaada kutoka kwa wadau mbalimbali vikiwa vimefungwa havitumiki.

Aliamuru
magodoro hayo yawekwe katika baadhi ya vitanda kwenye wodi ya uzazi na
vitanda vya kuhudumia wagonjwa wa kawaida vipelekwe kwa wagonjwa wa
kawaida.
Hata
hivyo alieleza kuwa ataendelea kutatua na kusimamia changamoto
zinazowakabili wananchi wa jimbo hilo katika sekta ya afya,maji,elimu na
kusaidia makundi maalum ikiwemo vijana,walemavu ,wanawake na wazee.
Nae
kaimu mganga mkuu halmashauri ya wilaya ya Kibaha,Grace Boniface
alisema amepokea malalamiko hayo na watasimamia maadili yanayotakiwa
kitaaluma .
Alikemea
tabia za kutoa siri za wagonjwa na kusema endapo watakwenda wanafunzi
wauguzi kituoni hapo kuanzia sasa,’ ni lazima kuwapa elimu na
kuwarejesha katika maadili ya kazi hiyo ili kuepukana na matatizo hayo.
Grace alisema kila mtumishi atimize wajibu wake na ambae atashindwa basi atabeba mzigo wake mwenyewe kwani atalazimika kuondolewa kuondolewa kwenye nafasi yake.
Kwa upande wake mganga mfawidhi wa kituo cha afya Mlandizi,Dkt Mpola Tamambele aliwataka watumishi kuendeleza umoja, upendo na mshikamano katika kuwapatia
huduma wagonjwa wanaofika kituoni hapo .

Alitaja
baadhi ya changamoto zinazowakabili kuwa ni sanjali na uhaba wa maji
hasa wodi ya uzazi ,gloves ngumu katika wodi hiyo na ukosefu wa mashine
ya kufulia hali inayosababisha kufua kwa kutumia mikono.
Dkt
Tamambele alitaja tatizo jingine ni uhaba wa madawa,vitanda vya kulazia
wagonjwa ambavyo vingi ni vibovu na uhaba wa wodi ikiwemo ya akinamama
na akina baba.
Ukosefu
wa uzio hali inayopelekea watu kupita ndani ya kituo na kupelekea
usumbufu kwa wagonjwa na kituo kudai kwamba kituo hicho ni kikubwa
,kinahudumia wagonjwa wengi hususan wa ajali za barabarani hivyo
kinapaswa kupandishwa hadhi na kuwa hospitali ya wilaya.
Dkt Tamambele alisema awali kulikuwa na upungufu mkubwa wa vifaa tiba na mashine za kupimia magonjwa lakini kwa sasa kituo kinatoa huduma ya kupiga picha mionzi (utra sound) na kupima presha na kisukari.
Akijibu kuhusu kutotumia vitanda vya kupimia wagonjwa vilivyotolewa msaada na NMB alisema ,kweli wana upungufu wa vitanda hivyo lakini walifuata maelekezo kutoka juu.
Kituo cha afya Mlandizi kinahudumia zaidi ya wagonjwa 35,000 kwa mwezi kutoka wilaya ya Kibaha na maeneo jirani .

Tags
AFYA