|
Mwanasheria na msemaji wa kampuni ya uchimbaji dhahabu ya RZ Frances Kiganga ,akielezea chanzo cha mgodi huo kujifunika.
IMEANDALIWA NA MADUKAONLINE
WATU kumi na nne(14)mmoja akiwa ni
Raia wa China wamefukiwa na udongo usiku wa kuamkia leo majira ya saa
saba usiku (7:00)wakiwa wanaendelea na majukumu yao ya uchimbaji kwenye
kampuni ya RZ Iliyopo kijiji cha Nyarugusu wilayani na Mkoa wa
Geita.
Sababu za kuporomoka udongo ni
kutokana na mgodi kuchimbwa zamani na Wajerumani hivyo kupelekea baadhi
ya maeneo hayo kuwa na nyufa na vyuma kushindwa kushikilia udongo wa
juu hali ambayo imepelekea kuzidiwa na mwisho wa siku kuporomoka.
Kamati ya ulinzi na usalama ya
Mkoa wa Geita,ikiongwaza na mkuu wa Mkoa huo Meja jenerali mstaafu
Ezekiel Kyunga imefika katika Mgodi wa RZ kuangalia na kujionea zoezi
la ukoaji .
Kamisha msaidizi wa madini kanda
ya ziwa victoria Mhandisi Yahaya Samamba ,ameelezea kuwa jitihada
ambazo zimefanyika ni kuwasiliana na migodi iliyopo karibu na eneo hilo
na pia wameshaomba msaada Kahama na kwenye mgodi wa GGM kupatiwa vifaa
vya uokoaji ili zoezi hilo liwezekufanikiwa kwa urais zaidi.
“Jitihada ambazo tumezifanya hadi
sasa tumeomba msaada kahama na kwenye mgodi wa Geita,kupatiwa vifaa
ambavyo vitasaidia kwa wepesi zoezi hili la uokoaji ingawa tumeshapata
vifaa vingine kutoka kwenye mgodi wa Busolwa”Alisema Samamba.
Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na
uokoaji Mkoa wa Geita.Elisha Mugisha,amesema kuwa eneo la chini ambalo
limefukiwa na udongo ndio ambalo kwa sasa wanaendelea kulitanua ili
sehemu hiyo iwe kubwa watu waweze kupita.
“Eneo lote lile la chini
limefukiwa na udongo lakini kule chini kunaonekana kuna sehemu za
kwenda pembeni ingawa limefukiwa lakini chini kunauhimala kunauwezekano
kule chini wale watu wapo hai na wamepelekewamipira ya hewa na kazi
inayofanyika ni kutanua eneo ambalo litasaidia kuwatoa watu
hao”tumekwisha kupeleka mipira
Mwanasheria na msemaji wa kampuni
ya uchimbaji dhahabu ya RZ Frances Kiganga ameelezea kuwa chanzo
kikubwa ni mashimo ya zamani kwani udongo unapotikisika umekuwa
ukisababisha baadhi ya nyufa kuendelea kupata shida.
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni
hiyo Charles Julius Na Robert Stanleyambao wameeleza kuwa mida ya saa
saba usiku duara lilinza kushuka taratibu na baada ya hatari hiyo
walipewa taarifa ya watu ambao walikuwa chini kupandisha juu lakini hata
hivyo jitihada hizo hazikuzaa matunda.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga amewataka wanaosimamia zoezi la uokoaji kuongeza nguvu ya uokozi .
Hadi Madukaonline inaondoka kwenye
eneo la tukio akuna mtu yoyote ambaye ameokolewa ingawa jitihada bado
zinaendelea kwa kuomba mashirika kuweka msaada zaidi wa uokoaji.
|