Wakazi wa Kijiji cha Kinywang’anga Mkoa wa Iringa wakiwa na hati zao za
umiliki wa ardhi mara baada ya kukabidhiwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba
na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi (aliyevaa miwani)
akifuatiwa na Mkurugenzi wa Shirika la Misaada la Watu wa Marekani
(USAID) Ndugu David Thompson na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Richard Kasesela.
Baadhi ya hati miliki za ardhi zikiwa zinaandaliwa ili kugawiwa kwa wananchi wa Kijiji cha Kinywang’anga Mkoani Iringa.
Ndugu
Yohanes Keng’ena na Mkewe Elizabeth Makang’olo wakipokea hati miliki ya
ardhi kutoka kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Mheshimiwa William Lukuvi.
Bibi
Catherine Abdallah akipokea hati miliki ya ardhi kutoka kwa Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi.
Ndugu Petro Wilson na Mkewe Leila Mlawa wakipokea hati miliki ya ardhi
kutoka kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa
William Lukuvi.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William
Lukuvi akiongoza ukataji utepe katika ufunguzi wa masijala ya ardhi ya
kijiji cha Kinywang’anga Mkoa wa Iringa.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William
Lukuvi akiongoa na wakazi wa Kijiji cha Kinywang’anga Mkoani Iringa.
Mkurugenzi
wa Shirika la Misaada la Watu wa Marekani (USAID) Ndugu David Thompson
akiongoa na wakazi wa Kijiji cha Kinywang’anga Mkoani Iringa.
Moja ya shamba la mkazi wa Kijiji cha Kinywang’anga Mkoani Iringa.
…………….
Na Hassan Mabuye (Kitengo cha Mawasiliano Serikalini – Wizara ya Ardhi)
Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi amewakabidhi hati miliki
810 za ardhi kwa wananchi wa Kijiji cha Kinywang’anga kilichipo Mkoani
Iringa.
Wananchi hawa wamekabidhiwa hati
hizo za umiliki wa ardhi baada ya kupimiwa maeneo yao ya viwanja na
mashamba wanayoyamiliki na kuandaliwa hati miliki ambazo walikabidhiwa
na Waziri wa Ardhi Mheshimiwa William Lukuvi kijijini hapo.
Katika tukio lingine Mheshimiwa
William Lukuvi amezindua masijala ya ardhi ya kijiji cha Kinywang’anga
Mkoa wa Iringa ili kuboresha huduma ya utoaji na uhifadhi wa hati miliki
za ardhi.
Akizungumza na wakazi wa Kijiji
hicho mara baada ya kuwakabidhi hati miliki zao za ardhi na kuzindua
baraza hilo Waziri Lukuvi aliwasihi wananchi hao kuzihifadhi na
kuzitunza hati zao hizo ili kuepukana na migogoro ya ardhi inayowakabili
wananchi wengi wasio na hati miliki nchini.
Nae Mkurugenzi wa Shirika la
Misaada la Watu wa Marekani (USAID) walioshirikiana na Serikali
kuwezesha uandaaji wa hati miliki hizo Ndugu David Thompson amemshukuru
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi
kwa kuja na kuwakabidhi Wananchi hati hizo na kuwaombaa Wananchi
kuzitumia kwa maendeleo yao.
Wananchi wa Kijiji cha
Kinywang’anga wamemshukuru Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi Mheshimiwa William Lukuvi pamoja na shirika la USAID
linaloendesha mradi wa ‘Tanzania Land Tenure Assistance’ kwa kuwaaezesha
kupata hati hizo maana ilikuwa kero kubwa katika kata yao.
Aidha, Waziri wa Ardhi ametoa hati
miliki hizo ili kutekeleza Programu ya Kitaifa ya kupima na kumilikisha
ardhi na kuzuia migogoro ya ardhi yenye lengo la kutekelezwa nchi
nzima. Utekelezaji huu utahusisha kuhakiki mipaka ya Mitaa na Vijiji
pamoja na maeneo mengine yote nchini na kupima kila kipande cha ardhi
kwa lengo la kumilikisha ardhi hiyo kwa wananchi, taasisi na Kampuni.
Sambamba na hilo, Matangazo ya
Serikali yanayotambulisha mipaka ya mikoa, Wilaya, Hifadhi za Taifa na
vijiji yatafanyiwa marekebisho baada ya mipaka yote nchini kuhakikiwa na
kukamilika.
Aidha mpango huu unalenga
kuwaunganisha wadau wa sekta ya ardhi katika kupanga, kupima, na
kumilikisha ardhi nchini na kuweka kumbukumbu za vipande vya ardhi ili
kuongeza thamani ya ardhi na kuondoa migogoro ya ardhi kwa ajili ya
maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Serikali ya awamu ya tano imeweka
adhma ya kumaliza migogoro ya ardhi iliyopo sasa na kuzuia kasi ongezeko
la migogoro ya ardhi ndani ya miaka mitano kwa kuandaa mpango kabambe
wa matumizi na usimamizi wa ardhi kwa kuharakisha na kurahisisha
upatikanaji wa hati za umiliki wa viwanja na mashamba.
Tags
HABARI KITAIFA