Ligi
kuu ya soka nchini Kenya inatarajiwa kuwa na timu kumi na nane kutoka
timu kumi na sita kuanzia msimu ujao baada ya kampuni inayosimamia ligi
hiyo KPL na shirikisho la soka nchini Kenya FKF kuafikiana.
Pande hizo mbili zimekuwa
zikitofautiana kwa muda kuhusu idadi ya timu zitakazoshiriki kwenye ligi
tangu msimu uliopita na kusababisha kucheleweshwa kwa tarehe ya kuanzi
kwa ligi.
Makubaliano hayo yaliafikiwa usiku
wa kuamkia leo baada ya bodi ya kusikiliza malalamishi kwenye michezo,
SDT, kuzipa pande hizo muda.
Hatua hiyo inaonekana kuwa ushindi
kwa Rais wa shirikisho la soka nchini FKF, Nick Mwendwa ambaye amekuwa
akitetea kuongezwa kwa idadi ya timu kwenye ligi hiyo.
Ingawa kampuni inayoendeesha ligi
hiyo, KPL, imekuwa ikipinga hatua hiyo kutokana na kutokuwepo kwa pesa
za kutosha, shirikisho hilo la soka limeahidi kutatua kikwazo hicho ili
kufanikisha uamuzi wa kuwa na timu kumi nane kwenye ligi.
Awali shirikisho la soka
liliziondoa timu tatu za Muhoroni Youth, Thika United, na Sofapaka kwa
kutokamilisha usajili wao wa kutimiza masharti ya usajili na leseni za
vilabu kulingana na FIFA na kusalia na timu 15.
Makubaliano hayo yamepatia
matumaini timu hizo zilizopigwa upanga kuanzisha upya mikakati ya
kusajiliwa tena ili kurejea kwenye ligi.
Maafisa wakuu watendaji wa KPL na
FKF wanatarajiwa kuwa na vikao zaidi kuziba pengo la pesa na masuala
mengine ya timu kwani shirikisho la FKF limeamua kutoka shilingi m
Tags
MICHEZO KIMATAIFA