Klabu ya soka ya Simba SC nayo imeungana na wapinzani wao Yanga kukataa
kucheza mechi ya kirafiki na mabingwa wa Afrika Mamelodi Sundown kutoka
Afrika Kusini.
Kwa mujibu wa mmoja wa viongozi wa Simba, amekiambia kipindi cha Sports
HQ cha EFM, hawatacheza mechi hiyo katikati ya wiki hii na mabingwa hao
kutokana na kubanwa na ratiba za ligi kuu ya Tanzania Bara.
Naye mratibu wa ziara ya mabingwa hao hapa nchini, Rahim Zamunda amesema
wamepanga timu hiyo ya Mamelodi kuanza kucheza mechi ya kwanza na Azam
FC Jumatano hii na alikuwa haoni sababu ya timu za Simba na Yanga
kukataa bahati hiyo kwa kuwa hata Barcelona wiki chache zilizopita
ilikuwa nchini Qatar wakati ligi yao bado inaendelea.
Mamelodi Sundown walikuja nchini kwa ajili ya ziara ya kupinga mauaji ya
tembo ambapo walipangiwa kucheza na timu za Yanga, Simba na Azam FC.
Tags
MICHEZO KIMATAIFA
