Waamuzi wa Uganda wameteuliwa kusimamia mapambano ya raundi ya kwanza ya
Ligi ya Mabingwa Barani Afrika inayoanza Mwezi Februari mwaka huu.
Kamati ya waamuzi ya CAF, imewateua, Mashood Ssali, Hussein Bugembe,
Musa Balikoowa Ngobi na Ali Sabila Chelegat kwa ajili ya mchezo wa
Zimamoto dhidi ya Ferroviara da Beira, ya Msumbiji, utakaopigwa Februari
pili mwa huu, 2017.
Kwa upande wa Tanzania Bara, Alex Muhambi, Ronald Katenya, Okello Lee na
Brian Miiro Nsubuga wameteuliwa kusimamia mchezo wa Yanga dhidi ya
Ngaya Club De Mde, ya Comoro, wikiend ya Februari 17 -19, 2017.
Tags
MICHEZO KIMATAIFA
