Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri Akiongea na watumisi wa Tume ya Mipango (hawapo pichani) wakati wa mkutano wake na watumishi hao. Kulia ni Naibu Katibu Mtendaji anayesimamia Klasta ya Sekta za Uzalishaji Bw. Maduka Kessy na wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu Bw. Abdulrahman Mdimu akifuatiwa Naibu Katibu Mtendaji, Klasta ya Biashara za Kimataifa na Mahusiano ya Uchumi, Bw. Paul Sangawe.
Kaimu Katibu Mtendaji, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri akiongea jambo na Naibu Katibu Mtendaji, Klasta ya Sekta za Uzalishaji Bw. Maduka Kessy wakati wa mkutano na watumishi wa taasisi hiyo.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mipango na Ufuatiliaji, Bw. Omary Abdallah akitoa taarifa fupi ya utekelezaji wa majukumu ya Tume ya Mipango katika kipindi cha nusu mwaka, kuanzia Mwezi Julai hadi Disemba kwa mwaka wa fedha 2016/17.
Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu Bw. Abdulrahman Mdimu akiwasilisha mada juu ya maadili kwa watumishi wa umma katika mkutano uliowahusisha wafanyakazi wa Tume ya Mipango.
Mwanasheria wa Tume ya Mipango, Bibi Nyanzala Nkinga akichangia jambo katika mkutano wa wafanyakazi wa Tume ya Mipango.
Watumishi wa Tume ya Mipango wakifuatilia kinachoendelea wakati wa mkutano uliofanyika katika ofisi za taasisi hiyo.
Watumishi wa Tume ya Mipango wakifuatilia kinachoendelea wakati wa mkutano uliofanyika katika ofisi za taasisi hiyo.
Watumishi wa Tume ya Mipango wakifuatilia kinachoendelea wakati wa mkutano uliofanyika katika ofisi za taasisi hiyo.
Watumishi wa Tume ya Mipango wakifuatilia kinachoendelea wakati wa mkutano uliofanyika katika ofisi za taasisi hiyo.
Watumishi
wa Tume ya Mipango wakifuatilia kinachoendelea wakati wa mkutano
uliofanyika katika ofisi za taasisi hiyo.PICHA ZOTE NA ADILI MHINA, TUME
YA MIPANGO
…………………………………………………………………………………………
Na Adili Mhina, DSM.
Katika kuitikia na kutekeleza
agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe
Magufuli la Serikali kuhamia Dodoma, Tume ya Mipango inatarajia kuanza
kuhamisha watumishi wake kuelekea Makau Makuu ya Nchi ifikapo mwezi
Machi Mwaka huu.
Taarifa hiyo imetolewa na Kaimu
Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri alipokutana na
watumishi wa taasisi hiyo Ijumaa Januari 26, 2017 kwa lengo la
kujadiliana mambo mbalimbali yanayohusu taasisi hiyo.
Pamoja na agenda zingine
kujadiliwa katika kikao hicho, suala la kuhamia Dodoma lilionekana
kuchukua nafasi kubwa miongoni mwa wafanyakazi mara baada ya ratiba ya
zoezi hilo kutolewa rasmi ambapo wengi walionesha kufurahishwa na
kutendo cha kutimiza ahadi ya Rais kwa wananchi ya kuhamia Dodoma.
Mwanri alieleza kuwa Tume ya
mipango itahamisha watumishi wake katika awamu tatu ambapo makundi
mawili yanatarajiwa kuhamia Dodoma ndani ya mwaka huu.
“Kundi la kwanza kwa upande wa
Tume ya Mipango litaondoka mwezi Machi mwaka huu ambapo pamoja na mambo
mengine, watumishi wa kundi hili watakuwa na jukumu la kuandaa mazingira
kwa ajili ya kuwapokea watumishi wengine watakaohamia baadae,” alisema
Mwanri.
Aliongeza kuwa sehemu ya pili ya
watumishi inatarajiwa kwenda Dodoma kuanzia mwezi Septemba mwaka huu
ambapo pamoja na watumishi wengine, kundi hilo linajumuisha Mkuu wa
Taasisi ambaye ni Katibu Mtendaji akiambatana na Wakuu wa Klasta, Idara
pamoja na Vitengo na kundi la mwisho linatarajiwa kuhama kuanzia mwezi
Machi, 2018.
Kikao hicho pia kilitoa fursa ya
kutolewa kwa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Tume ya Mipango
katika kipindi cha nusu mwaka, kuanzia Mwezi Julai hadi Disemba kwa
mwaka wa fedha 2016/17.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya
Mipango na Ufuatiliaji, Bw. Omary Abdallah alieleza kuwa katika Kipindi
hicho Tume ya Mipango imefanikiwa kutekeleza majukum mbalimbali ikiwemo;
kuandaa mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2017/18
na kuendesha mafunzo kuhusu mwongozo wa usimamizi wa Uwekezaji wa Umma
katika ngazi ya Sekretarieti za mikoa na mamlaka za Serikali za mitaa
nchini.
Mafanikio mengine ni kuendelea
kusambaza Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2016/17 –
2020/21) kwa wadau pamoja na kuendelea kuandaa mikakati minne ya
utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa unaendelea (Mkakati
wa utekelezaji, Ugharamiaji, Mawasiliano na Ufuatliaji na Tathmini).
Aidha Tume ya Mipango ilifanikiwa
kufuatilia utekelezaji wa baadhi ya Miradi ya Maendeleo ya Kitaifa
katika mikoa ya Mwanza, Dodoma, Tabora, Mtwara, Lindi, Pwani na Dar es
salaam kwa lengo la kutathmini maendeleo ya utekelezaji wa miradi na
kuelewa changamoto zinazokabili utekelezaji wa miradi hiyo.
Tags
HABARI KITAIFA