Mbunge wa jimbo Bagamoyo, dk.
Shukuru Kawambwa, akishukuru baada ya shule ya msingi Nianjema kupokea
madawati 60 kutoka kwa shule za Feza na wadau, taasisi ya Time To Help .
Mwalimu mkuu msaidizi wa shule ya
msingi Nianjema, Bagamoyo, Ally Swalehe akipokea madawati 60 kutoka kwa
mkurugenzi wa shule za Feza, Ibrahim Yunus.
Mkurugenzi wa shule za Feza
Ibrahim Yunus akizungumza na walimu na wanafunzi wa shule ya msingi
Nianjema na kabla ya kuwakabidhi madawati 60 aliyochangia kwa
kushirikiana na taasisi ya Time To Help.
(picha na Mwamvua Mwinyi)
Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
Mkurugenzi wa shule za
Feza Ibrahim Yunus kwa kushirikiana na taasisi ya Time to Help wametoa
msaada wa madawati 60 yenye yaliyogharimu mil. 10 kwa shule ya msingi
Nianjema,Bagamoyo .
Akikabidhi madawati hayo,Yunus alisema ,lengo ni kusaidia kukabiliana na changamoto ya upungufu wa madawati shuleni hapo.
Alisema pia yatawezesha kuondoa tatizo la kukaa chini kwa wanafunzi hao na kusoma katika mazingira bora.
Aidha Yunus alieleza
kwamba kuanzia sasa shule za feza zitakuwa rafiki wa shule ya msingi
Nianjema na kusaidia kusomesha wanafunzi watakaofaulu mitihani ya darasa
la saba.
“Fanyeni kama ilivyo kwa shule zangu ambazo zimeongoza kwa kutoa mwanafunzi wa kwanza na kuwa shule ya kwanza kitaifa”
“Madawati haya
wamechanga watu wa kawaida na kwa kushirikiana na shirika dada la Time
To Help,naamini itakuwa chachu katika kuinua taaluma “alisema Yunus.
Katibu mkuu wa Time to
Help, Ibrahim Ebrahim,alisema jukumu la kutatua changamoto za sekta ya
elimu ni la jamii,wadau pasipo kuiachia serikali pekee.
Nae mbunge wa jimbo la Bagamoyo na Waziri wa zamani wa Elimu,dk Shukuru Kawambwa alishukuru kupata msaada huo .
Alisema madawati hayo 60
yatakaliwa na wanafunzi watatu kila dawati hivyo kuwaondolea adha
wanafunzi 180 waliokuwa hawana madawati.
Dk Kawambwa alisema kuwa madawati hayo yatasaidia kuhakikisha wanafunzi wanakaa kwenye madawati ambapo wataweza kuandika vizuri.
Kaimu mwalimu mkuu wa
shule hiyo Ally Swalehe alisema ,wanakabiliwa na upungufu wa madawati
287 huku shule hiyo ikiwa na wanafunzi 2,168 .
Alisema changamoto
nyingine ni ongezeko la uandikishwaji wa wanafunzi kutokana na mfumo wa
elimu bure ambapo uandikishaji umefikia asilimia 32 na kusababisha
msongamano wa wanafunzi
Tags
ELIMU