Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuwa hatua kali zitachukuliwa kwa
atakayepokea rushwa kutoka kwa wauzaji, wasambazaji na watumiaji wa
madawa ya kulevya.
Ameyasema hayo jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa kikao cha
kwanza cha Baraza la Taifa la kudhibiti dawa za kulevya nchini.
“Sheria ya udhibiti wa madawa ya kulevya itumike vizuri, Serikali na
Baraza halitahitaji mtu yeyote mwenye mamlaka kupokea rushwa
ikigundulika hatua kali zitachukuliwa,” amesema.
Waziri Mkuu alisisitiza kuwa Serikali imedhamiria kuendelea kuimarisha
mapambano dhidi ya udhibiti wa dawa za kulevya nchini ambayo yamekuwa
yakifanywa na Serikali zilizotangulia
Tags
BIASHARA HARAMU
