
Beki wa Zambia 'Chipolopolo', Stoppila Sunzu amesaini mkataba wa miezi
mitano wa kuichezea klabu ya Arsenal Tula inayoshiriki Ligi Kuu Russia.
Taarifa zinasema kuwa Sunzu, ambaye ni mchezo wa Lille ya Ufaransa, amesaini mkataba huo na Tula akiwa Uturuki ilipoweka kambi.
Kwa mujibi wa wakala wa mchezaji huyo Nir Karin amesema mkataba huo
utamfanya Mzambia huyo kucheza Russia hadi Juni 2017 na baada ya hapo
atarejea Lille ambako mkataba wake utamalizika 2019.
Taarifa zinadai kuwa Sunzu alikuwa anatakiwa Ubelgiji, United Arab
Emirates, Marekani na Uturiki, lakini klabu hiyo ya Russia ilionyesha
kumtaka zaidi.
“Tumechagua Russia na kuziacha Ureno, Uturuki na Marekani kwa sababu
hapa kuna ligi yenye ushindani zaidi. Na Juni akimaliza kucheza kwa
mkopo atarudi moja kwa moja Lille,” anasema Karin.
Sunzu tayari ameshazichezea klabu za Konkola Blades, Zanaco, Chateauroux
na TP Mazembe kabla ya kuhamia Sochaux ya Ufaransa na Shanghai Shenhua
ya China msimu wa 2015.
Tags
MICHEZO KIMATAIFA