Juzi kati Waziri wa Katiba na Sheria Dr.Mwakyembe alisikika kupitia
kipindi kimoja cha "East Africa Tv/Radio" akilalamika jinsi
alivyomshindwa Masogange katika vita vya madawa ya kulevya.Dr Mwakyembe
anasema hata baada ya ushahidi wote kuonyesha kuwa "mzigo" ulipitishwa
hapa Dsm kuelekea J'burg,lakini bado Masogange alimponyoka.
Anasema,baada ya muda,alihamishwa ktk Wizara hiyo na kupelekwa sehemu
nyingine,kitu kilichomfanya ashindwe kuendeleza harakati za vita
hiyo.Sisi tutamuamini Dr kwa yale anayoyasema,wengi wanaomfahamu
wanasita kumuamini.
Lakini haya yote,hayaondoi ukweli kuwa,Dr Mwakyembe,daktari wa
sheria,mwanazuoni,wakili,Waziri na Mbunge wa Jimbo la Kyela,alielemewa
na Masogange mpaka akawa anamletea "nyodo".
Mjadala mkubwa aliouibua Dr Mwakyembe,ni huyo "kijana" wake aliyekuwa
"anamsaidia" katika vita hivi,bahati nzuri au mbaya,licha ya kusema
"kijana" wake anatakiwa alindwe huko gerezani,bado Dr aliamua kumtaja
kwa jina moja la JINGU,hivyo aliotoa mwanya wa kudadisi;Huyo "kijana
wake Jingu ni nani haswa?"
Dr Mwakyembe hajasema huyo "kijana" wake alifungwa kwa kosa gani
hasa,yeye kama mwanasheria na waziri,ametumia njia gani za kisheria
kuhakikisha huyo "kijana" wake anatoka huko gerezani?Na je Mwakyembe ana
uhakika kuwa huyo "kijana" wake aliomsaidia kwa 99% ni kweli yupo huko
gerezani kwa "kubambikiwa" au ni stahili yake.
Na je,kukamatwa kwake huyo "kijana" kuna uhusiano wowote na "msaada" kwa
Dr Mwakyembe?Au kukamatwa kwake "kunahusishwa" tu,lakini kuna jambo
lingine tofauti na "msaada" huo kwa Dr?
Clemence Jingu Mbaruck (bila shaka ndio huyu "kijana" wa Dr Mwakyembe)
alikuwa Meneja wa Usalama (Manager Security) wa Mamlaka ya Viwanja vya
ndege Tanzania.Alihudumu kwa nafasi andamizi kabla ya cheo hicho katika
kitengo cha Usalama katika uwanja wa Julius Nyerere kwa muda mrefu.
Kwa maelezo ya Kamishna Rogers Sianga,moja ya mbinu kubwa ya "drug
lords" ni ku-recruit watu ktk kila kitengo wanachopita ili iwe rahisi
kwao kupitisha mizigo yao,kitengo cha usalama ktk viwanja vya ndege,ni
moja ya "waajiliwa" wa mitandao hii.Hivyo hawa huwa na "details" za
lini,saa ngapi,nani,na ndege gani itapitisha mzigo kuingia au kutoka nje
ya nchi.
July 2015,mzigo wa kilo 262 wa pembe za ndovu ambao ni sawa na tembo 50
ulikamatwa katika uwanja wa ndege wa Zurich Uswis,ukiwa umetoka Dsm
kuelekea China.
Mzigo huo ulikamatwa ukiwa ndani ya begi za raia wa China.Begi hizo
zilipita bila kuonekana Tanzania, iwe kwa macho au kwa "Screening
machine".
Soma Nyara za Serikali zawafikisha kizimbani Maafisa 4 wa TAA
Watuhumiwa wanne ambao ni wafanyakazi wa Kitengo cha Usalama wakiwemo
wanajeshi watatu wa JWTZ (ambao huwa wapo attached ktk kitengo cha
usalama wa kiwanja) na Manager Security Jingu walitiwa kizuizini kwa
tuhuma za kuhisika kufanikisha mzigo huo kupita bila kukamatwa.
Clemence Jingu (kijana wa Mwakyembe) na wenzake waliwekwa mahabusu kwa
tuhuma ya Uhujumu uchumi,na kesi yao kusomwa mahakama ya Kisutu na
baadae kurudishwa rumande sbb kesi hii haina dhamana.
Mpaka leo,Jingu yupo ndani akiendelea kusota kutokana na kesi hii.Ni
kesi inayotambulika kama ya "Uhujumu Uchumi" ambayo haina
dhamana.Kukamatwa kwa Jingu kulitokana na nafasi yake kama "Manager
Security" ambaye inaonekana (sababu mahakama haijathibitisha) alishiriki
kufanikisha mzigo huo kupita bila kizuizi.
Huwezi kupita na mzigo wa kilo 262 wa meno ya tembo bila kuonekana kwa
macho wala kwa mashine.Ni lazima uwe na mtandao wa maana utakaorambishwa
"asali".Mtandao huu wa kuramba "asali" hauishii kwa "security officers"
wanaokagua mizigo magetini tu,ni lazima ufike mpaka kwa "boss".Na
pengine swali lilikuwa,"mzigo mkubwa kama huu unaweza kupita bila
Manager Security kujua?"
Leo Dr Mwakyembe,wakili,Waziri na Mbunge,bila kujali usiri wa taarifa za
mtoa taarifa kaamua kututajia hadharani mtu aliyekuwa anamsaidia kwa
99%.Tena kwa kumtaja ktk chombo cha habari.Lakini sidhani kama
amejiridhisha kuwa kuwekwa ndani kwa "mtoa taarifa" wake ni kweli kwa
sbb ya vita ya madawa ya kulevya?
Na hata kama ni hivyo,Je Dr hana namna ya kisheria iwe kwa kumuwekea
mawakili au msaada wowote wa kisheria kuhakikisha "kijana" wake
anatoka!?Na ana uhakika kuwekwa ndani kwa Jingu ni sbb ya "uadui wa
kutoa ushirikiano wa 99%?".
Zaidi ya hapo,Dr ametuonyesha kuwa hana "kifua",inawezakana huyo
"kijana" wake alikuwa anampa habari hizo sbb ni Waziri na bosi wake,sasa
inakuwaje leo aamue kutaja chanzo chake cha habari kwa jina na mahali
alipo?Alipoamua kumtaja Jingu hadharani,alitupa nafasi ya kudadisi;huyo
Jingu "kijana" wa Mwakyembe ni nani?
Leo Masogange na washirika wake na wote waliokamatwa enzi za Mwakyembe
kupitia uwanja wa JNIA,wanajua Jingu ndio aliowachoma.Hali hii ya kukosa
"kifua" cha kutunza siri unazopewa ktk uwajibikaji,haiwezi kuwakatisha
tamaa maafisa wengine wa JNIA katika vita hivi vya sasa?
Maana kwa kauli hii ya Dr,ni wazi kuwa hata maafisa wengine wa usalama
JNIA wanaweza kuogopa kutoa taarifa kwa kuhofia siku moja huko mbele ya
safari mtu atakuja kutaja chanzo chake cha habari.
Tags
BIASHARA HARAMU
